[caption id="attachment_38787" align="aligncenter" width="750"] Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji (Mstaafu), Mary Longway akifungua mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge utakaodanyika katika jimbo la Temeke na Udiwani katika kata 46 za Tanzania Bara jijini Dodoma.[/caption]
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka Wasimamizi wa Uchaguzi kuzingatia kanuni,sheria na miongozo ya Uchaguzi wanaposimamia na kutekeleza majukumu ya uchaguzi.
Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh. Jaji Mstaafu Mery Longway katika ufunguzi wa mafunzo kwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi yaliyofanyika Mkoani Dodoma leo.
Ameeleza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndio yenye jukumu la kusimamia , kuendesha na kuratibu Uchaguzi , lakini wanaosimamia jukumu hilo kwa ukaribu zaidi ni wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo , Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo, Wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata pamoja na Watendaji wa vituo vya kupigia Kura.
“Nawakumbusha kuzingatia kanuni, Sheria na Miongozo yote iliyotolewa na itakayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kusimamia jukumu hili kwa ufanisi na mafanikio makubwa”. Amesema Mh. Longway.
Aidha amewakumbusha wasimamizi hazo wa Uchaguzi kuwa Uchaguzi ni Mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali za kufuatwa na kuzingatiwa ndio msingi wa Uchaguzi kuwa huru wa haki na kupunguza kama siyo kuondoa kabisa malalamiko au vurugu wakati wote wa Uchaguzi na hivyo kupunguza kesi mahakamani baada ya Uchaguzi.
Amesema kuwa pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo kuwa wazoefu katika kuendesha Uchaguzi washiriki hao wametakiwa kuhakikisha wanazingatia maelekezo watakayopewa na wakufunzi wa Tume, haitokuwa vyema kutekeleza majukumu hayo kwa mazoea bali wanatakiwa kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni zinazosimamia zoezi la Uchaguzi
Washiriki wa Mafunzo hayo ni Wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo , Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo, Wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata ambao watasimamia Uchaguzi Mdogo wa Umbunge Jimbo la Temeke na Udiwani katika kata 46 utafanyika Januari 19 mwaka 2019.