Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Nditiye Aitaka Sekta ya Mawasiliano Iongoze Kuchangia Pato la Taifa
Mar 18, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_51748" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Tawi la Mawasiliano wakati akifungua kikao cha Baraza hilo, Dodoma[/caption]

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amesema kuwa Sekta ya Mawasiliano ni sekta mtambuka ambayo ina mchango mkubwa katika kuinua pato la Taifa hivyo watendaji wake hawana budi kufanya kazi kwa bidii, ufanisi na kutoa huduma bora kwa jamii ili iwe ya kwanza katika kuchangia pato la taifa.

Mhandisi Nditiye ameyasema hayo alipokuwa anafungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano uliofanyika katika ukumbi wa Kituo Cha Mikutano Cha Dodoma mkoani Dodoma.

“Sekta ya Mawasiliano ni sekta ambayo taasisi za Serikali, sekta ya umma na binafsi zinategemea huduma za mawasiliano, sisi ndio wasimamizi na watunga sera ambapo tunahitajika kuhakikisha mawasiliano yanajitosheleza kwenye dunia ya kisasa ambayo inapelekea dunia kuwa kijiji kimoja”, amesema Mhandisi Nditiye.

  [caption id="attachment_51750" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Kitolina Kippa akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye kufungua Baraza la Wafanyakazi wa Sekta hiyo, Dodoma.[/caption]

Aidha, amesisitiza kuwa Sekta ya Mawasiliano ina uwezo wa kufanya vizuri zaidi katika kuchangia pato la taifa kwa kuwatumia vema wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wenye weledi na wabunifu ili waweze kuisaidia Serikali katika jukumu zima la kuwahudumia wananchi kwa kuwa Sekta hii imekuwa inaongoza kwa kuchangia pato la taifa katika kipindi cha mwaka 2017/2018 kwa kushika nafasi ya tatu ambapo imechangia asilimia 13.4 ya pato la taifa na imeendelea kuongoza na kuwa kati ya tano bora ya vyanzo vikuu vya mapato nchini.

Akizungumzia umuhimu wa Baraza la Wafanyakazi, alisema kuwa Baraza ni kiungo muhimu kuwezesha Menejimenti kutimiza majukumu yake na kusimamia mwenendo mzima wa utendaji kazi wa Wizara na Sekta kwa ujumla kwa mujibu wa majukumu yake hivyo ni vema kuhakikisha kuwa viongozi na watumishi wanashirikiana katika kutekeleza majukumu yao kwa kuwa kila mmoja anategemea uwepo wa mwingine

Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Kitolina Kippa amesema kuwa katika kikao hicho, wajumbe watapokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Sekta kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2019/2020 ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya TEHAMA na utoaji wa huduma za mawasiliano ndani ya Serikali na kwa wananchi ili kuhakikisha kuwa huduma zinapatikana kwa wakati na kwa uhakika; kupitia mipango iliyoandaliwa kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa majukumu ya Sekta kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021 pamoja na kutoa mafunzo ya kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu janga la UKIMWI, maambukizi ya magonjwa yatokanayo na lishe; na kuwataka watumishi wa umma kushirikiana kwa pamoja na kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma ili Serikali iweze kuwahudumia wananchi wake ipasavyo

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Tawi la Mawasiliano wakiimba wimbo wa wafanyakazi wa mshikamano daima “solidarity forever” wakati wa kikao cha Baraza hilo kilichofanyika Dodoma.Naye Mwenyekiti wa Wanawake wa Tawi la Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Grace Chalila ameuomba uongozi wa Wizara kuiomba Serikali iongeze bajeti ya Sekta ya Mawasiliano ili iweze kuchangia zaidi pato la taifa tofauti na inavyochangia sasa kwa kuwa watalaamu wapo na wanaweza kutoa huduma za mawasiliano kwa wananchi na Serikali yenyewe kwa kuzingatia kuwa Serikali inatumia na kutegemea kwa kiasi kikubwa matumizi ya TEHAMA na mifumo ya kielektroniki na huduma mtandao ikiwemo Serikali mtandao, elimu mtandao, afya mtandao na ukusanyaji wa kodi na mapato ya Serikali

Katika hatua nyingine, Mhandisi Nditiye amewakumbusha wafanyakazi kuwa ugonjwa wa UKIMWI upo na amewataka wajilinde na kujali afya zao kwa kuwa Serikali inawategemea katika kutekeleza majukumu yao ili waweze kuwahudumia wananchi

Vile vile, amewataka wazingatie maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya nchini kwa kuzingatia usafi na kuepuka kusalimiana kwa kutumia mikono na wanawe mikono kila wakati kwa kuwa virusi vya Corona vimeingia nchini na tayari imeripotiwa kuwa mwananchi mmoja amebainika kuwa na COVID 19

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyevaa tai aliyesimama mstari wa mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Tawi la Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi