[caption id="attachment_20770" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Viwanda, Biasahara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) (Hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi katika Makao Makuu ya Shirika hilo jana jijini Dar es Salaam.[/caption]
Na, Thobias Robert.
Naibu waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya ameitaka Bodi ya Shirika la Taifa ya Maendeleo (NDC) kuhakikisha kuwa inasimamia kwa ukamilifu na ufanisi miradi iliyopo chini ya shirika hilo ili ikamilike kwa wakati.
Naibu Waziri Mhandisi Manyanya aliyasema hayo jana alipofanya ziara ya kikazi katika Makao Makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam, ambapo aliiagiza bodi hiyo kuhakikisha kuwa miradi ya kufua chuma ya Liganga na Mchuchuma, mradi wa kuunganisha matrekta mkoani Pwani, pamoja na kusimamia kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tire mkoani Arusha vinafanya kazi.
“Ni wajibu wetu kufike mahali tuonyeshe kwa vitendo nini tunafanya, fanyeni kazi kwa vitendo mnayo miradi mikubwa ya nchi, nitafanya kazi na nyinyi usiku na mchana ili kuhakikisha kuwa miradi hii inatekelezwa,” alifafanua Mhandisi Manyanya.
[caption id="attachment_20773" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo Bw. Ramson Mwilangali akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Viwanda, Biasahara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya kufuatia ziara ya kikazi aliyoifanya Naibu Waziri huyo katika Makao Makuu ya shirika hilo jana Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_20774" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Viwanda, Biasahara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Maendeleo alipofanya ziara katika Makao Makuu ya shirika hilo jana jijini Dar es Salaam.[/caption]Aidha aliongeza kuwa ni wajibu wa NDC kuhakikisha kuwa wanazingatia sheria hususani ya kulinda rasilimali na kuhakikisha kuwa wawekezaji wote wanaosaini mikataba ya ujenzi na kuendeleza miradi iliyo chini yao wanazingatia sheria.
Aliongeza kuwa mataifa duniani kote yanategemeana hivyo ni lazima kuwepo na manufaa kwa wawekezaji, wananchi na serikali kwa ujumla na kuwaelezxa aliwahakikishia kuwa serikali itafanya kazi bega kwa bega na shirika hilo ili liweze kutatua changamoto zake na kukamilisha miradi hiyo.
“Inabidi mshikamane mfanye kazi kwa umakini zaidi ili kuhakikisha kuwa miradi hii inatekelezwa, wananchi hawana furaha na shirika la mendeleo msipokuwa makini hii meza yote siku moja hamtakuwepo hapa na nitakuta sura mpya kabisa nawapa salamu yenu,” alisisitiza Mhandisi Manyanya.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Bw. Ramson Mwilangali, alisema kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutainua na kuimarisha uchumi wa taifa na kutengeneza ajira nyingi kwa vijana na pamoja na mapato ya serikali.
Akizungumzia kuhusu mradi wa Liganga na Mchuchuma, Mwilangali alisema mradi huo utakuwa na vipengele vitano ambapo kipengele cha kwanza, ni mgodi wa kuzalisha makaa ya mawe tani milioni 3 kwa mwaka, kituo cha kuzalisha umeme wa megawati 600, na kipengele cha tatu ni msongo wa umeme KV 2200 kutoka mchuchuma kwenda Liganga,.
Anavitaja vipengele vingine kuwa ni cha nne mgodi wa chuma utakaokuwa Liganga na na kipengele cha tano ni kiwanda cha chuma kitakachojengwa Liganga.
Aidha aliongeza kuwa mradi huo unaotarajiwa kuanza kujenga mwakani utagahrimu dola za kimarekani bilioni 3.