Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

NBS na Sheria Mpya ya Utoaji Takwimu
Feb 28, 2019
Na Msemaji Mkuu

Na. Msafiri Ulimali, Fatma Athumani

Ofisi ya Taifa ya Takwimu –NBS imetoa maelezo ya marekebisho ya Sheria ya Takwimu Namba 9 ya mwaka 2015 katika ofisi za takwimu zilizopo barabara ya Sokoine jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano jana, Mkurugenzi Mtendaji wa NBS Dkt. Albinas Chuwa amesema kuwa sheria ya takwimu ya Mwaka 2015 imerekebishwa kupitia Sheria Namba 8 ya mwaka 2018.

Dkt Chuwa amesema “Lengo la marekebisho hayo, ni kuimarisha utaratibu wa usambazaji takwimu nchini, kwa nia ya kuepusha kutoa takwimu zinazokinzana kwa jamii, pia, marekebisho hayo yanalenga kuimarisha mijadala ya kisera pamoja na matokeo yake’.

Aidha, marekebisho ya sheria hiyo ambayo yamejikita zaidi katika kuweka utaratibu wa uchambuzi wa kina kutumia mfumo wa kuweka takwimu ‘Dataset’ zinazotokana na tafiti  kadhaa ambazo nyingi zimewekwa kupitia kwenye tovuti  ya NBS na baadhi zipo kwenye hifadhi zetu, amesema Dkt. Chuwa.

Akieleza utaratibu wa utoaji wa takwimu ambazo zitatofautiana na zilizotolewa awali na Ofisi ya takwimu  amesema kuwa ambapo ikitokea kuna matokeo yaliyowekwa na tofauti na yale yaliyotolewa na NBS katika kiashiria cha aina hiyo, marekebisho yanaweka utaratibu wa namna bora ya utoaji ya matokeo hayo.

Pamoja na hayo Dkt. Chuwa amesema kuwa marekebisho yamelenga zaidi kuondoa mkanganyiko kwa jamii  unaoweza kutokea iwapo zitatolewa takwimu zenye lengo la kupotosha takwimu zilizotolewa awali, takwimu za aina hii ni zile zimetolewa bila kufanyiwa utafiti wa kutosha,”

Kufuataia marekebisho hayo ya kitakwimu ya mwaka 2017 zimeanza kupitiwa ili kuwezesha utekelezaji wa marekebisho ya sheria ambapo kanuni zake zitatoa ufafanuzi wa namna bora ya utekelezaji wa matakwa ya kisheria.

Vilevile, Dkt Chuwa amesema “Marekebisho haya hayana lengo la kuingilia mchakato wa ukusanyaji wa takwimu ambazo zinakuswanya kwa matumizi ya ndani”.

Akitolea  mfano  katika kuelimisha umma  amesema kuwa sheria hii haina uhusiano kabisa na yule mtu anayekusanya takwimu zake au za taasisi yoyote kwa ajili yake na manufaa yake binafsi  amesisitiza Dkt Chuwa .

Naye,  Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Utafiti wa Kupunguza Umasikini -REPOA Dkt. Donald Mmari amesema kuwa sheria hii haina mambo mapya sana ila lengo kuu sana ni kutengeneza muongozo mzuri wa nchi, na uwepo wa ushirikiano WA REPOA na Taasisi ya NBS inayohusika na sheria ya takwimu nchini.

 “Sisi kama wadau wa takwimu na wazalishaji wakubwa wa takwimu tumekua tukishirikiana na Taasisi ya NBS tangu REPOA  ilivyoanzishwa mwaka 2001 kwa karibu sana ambapo tu watumiaji wakubwa wa takwimu zake”.

Aidha, akielezea suala zima la tafiti Dkt Mmmari amesema kuwa tumekuwa tukiulizana  maswali, wakati tukifanya mjadala wa methodolojia tunazotumia, wakati mwingine zinatuma majibu tofauti lakini yanaelezeka kwa kutolewa maelezo.

Akitoa ufafanuzi wa jambo hilo ameongeza kwa kusema, baadhi ya sheria na kanuni hizi hazikua na mambo mapya sana, zimetoa utaratibu mzuri zaidi, kupata taarifa na kuzalisha taarifa, lakini pia kushirikisha wananchi kuwapa matokeo ya tafiti mbalimbali zinazoendelea hapa nchini.

Pia, miongozo ya sheria ya kanuni hii zinaelekeza utafiti kutumia njia ambazo ni sahihi na bora zaidi ili kuweza kuwa na takwimu za kutosha, laikini ambazo zimekusanya kwa njia bora bila kufanya ubadhirifu wowote ule.

Mwisho Dkt. Mmari ameitaka Taasisi kutumia wadau mbalimbali muhimu akiwemo Waziri Mkuu katika tafiti za taasisi, huku akisisitiza kuwa tafiti hizo lazima ziwe za  viwango  bora za kufanya takwimu zote zifanane na kutumia njia ambazo zinakubalika kiusahaihi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi