[caption id="attachment_42668" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akitoa wito kwa wadau mbalimbali nchini kuandaa Mashindano ya kusaka vipaji vya Muziki kwa Vijana kuanzia ngazi ya Wilaya na Mkoa jana Mkoani Iringa alipokuwa akizindua Mashindano ya Kabati Star Search yaliyoandaliwa na Mhe.Ritha Kabati Mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa huo.[/caption]
Na Anitha Jonas - Iringa
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza ameto wito kwa wadau mbalimbali nchini kujitokeza kuandaa Mashindano ya kusaka vipaji vya Muziki kwa vijana kwa kuanzia ngazi za Mikoa na Wilaya.
Mheshimiwa Shonza ametoa wito huo jana Mkoani Iringa alipokuwa akizindua Tamasha la Ritha Kabati Star Search lililolenga kusaka vipaji vya vijana wanaojua kuimba muziki na tamasha hilo limekusanya vijana zaidi ya 150 kutoka maeneo mbalimbali ya wa Mkoa wa Iringa.
[caption id="attachment_42669" align="aligncenter" width="1000"] Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Iringa Ritha Kabati ambaye ndiye mwandaaji wa Mashindano ya Kabati Star Search akimweleza Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza(hayupo pichani) mpango wa kuhakikikisha washindi watatu wa mashindano hayo kuwa narekodi nyimbo zao na wasanii wa kubwa nchini kwa kushirikiana na mlezi wa Wasanii Bw.Said Fella maraafu kama Mkubwa Fella jana katika uzindizi wa mashindano hayo yaliyofanyika Manispaa ya Iringa.[/caption] [caption id="attachment_42661" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (watatu kulia) akiwasili katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha (RUCU) jana na kupokewa na vijana wanaoshiriki mashindano ya Kabati Star Search ambapo mashindano hayo yanafanyika hapo, watatu kushoto ni Ritha Kabati Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Iringa ambaye ndiye mwandaaji wa mashindano hayo.[/caption]“Ninapenda kumpongeza Mhe.Ritha Kabati Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa kwa kuandaa Tamasha lenye tija kwa taifa kama hili, pia ninaomba wadau mbalimbali wenye uwezo kuandaa matamasha kama haya kwa kuanzia ngazi za mbalimbali ndani ya mikoa na wilaya zetu kwa ndiko waliko vijana wenye vipaji, tuwasaidie kufikia ndoto zao kwa manufaa ya taifa,”alisema Mhe.Shonza.
Akiendelea kuzungumza katika uzinduzi huo wa Kabati Star Search Naibu Waziri huyo alimtaka Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Iringa kuandika barua kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ya kuomba wataalamu kuja kutoa mafunzo kwa wasanii chipukizi wa muziki wa mkoa huo kwa lengo la kuwa ongezea maarifa wasanii hao.
Naye muandaaji wa Tamasha hilo Mhe.Ritha Kabati alieleza kuwa amekuwa akiwaona vijana wa mkoa huo na kuwa wanavipaji ila wamekuwa wakikosa jukwaa la kuonyesha vipaji vyao na ndiyo maana aliamua kuanzisha mashindano hayo ambayo yatawainua vijana wa mkoa wa Iringa nao kuanza kusikika Kitaifa na Kimataifa kama wasanii wengine maarufu hapa nchini.
[caption id="attachment_42662" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (wapili kushoto) akisalimiana na mchekeshaji maarufu Baraka Mwakipesile anayeigiza kama Rais Magufuli ambapo kwa sasa anajulikana kama Baraka Magufuli mara baada ya uzinduzi wa mashindano ya Kabati Star Search yaliyofanyika jana Mkoani Iringa, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mufundi Bw.Netho Ndilito.[/caption] [caption id="attachment_42664" align="aligncenter" width="1000"] Mmoja ya washiriki wa mashindano ya Kabati Star Search Yahya Hamadi kutoka Kata ya Mwangata Mkoani Iringa akionyesha uwezo wake kwa kuimba wimbo wa Msanii Young Killer katika mashindano hayo yaliyofanyika jana ambapo yalizinduliwa na Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (hayupo pichani).[/caption]“Katika kuhakikisha mashindano haya yanaleta mafanikio nilizungumza na mmoja wa walezi wasanii wa Muziki nchini Bw. Said Fella Maarufu kama Mkubwa Fella kuhusu kuwasaidia washindi wa mashindano haya na tukakubaliana kuwa mshindi wa kwanza mpaka watatu atawachukua na kwenda kuwafunza vizuri kisha watarekodi nyimbo zao na pia wataimba na wasanii maarufu hapa nchini na atahakikisha na hizo nyimbo zao zinapigwa katika vituo vya redio na televisheni mbalimbali nchini,”alisema Kabati.
Pamoja na hayo Kabati alieleza kuwa vijana wa Iringa wamesema wanataka nao Mkoa wao uonyesha kuwa unavipaji vyenye uwezo mkubwa wakufikia ngazi za Kimataifa kwani kupitia mashindano ya mpira wa miguu ya Kabati Challenge Cup vijana watatu tayari wamechukuliwa na timu za mpira za Afrika Kusini kwa lengo la kwenda kuchezea timu za vijana na watakuwa wanasomeshwa huko pia .
[caption id="attachment_42665" align="aligncenter" width="1000"] Mmoja ya washiriki wa mashindano ya Kabati Star Search Sophia Kalinga kutoka Kata ya Gangilonga Mkoani Iringa akionyesha uwezo wake kwa kuimba wimbo wa You Raise Me Up kutoka kwa msanii Josh Groban katika mashindano hayo yaliyofanyika jana Mkoani hapo.[/caption] [caption id="attachment_42666" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (watatu kushoto ) akiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Shindano la Kabati Star Search mara baada ya uzinduzi wa shindano hilo lililofanyika jana Mkoani Iringa, wapili kushoto ni muandaaji wa shindano hilo Ritha Kabati Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Iringa .[/caption] [caption id="attachment_42667" align="aligncenter" width="1000"] Msanii wa Mkoa wa Iringa Ezra Msiliova maarufu kama Eze Nice akiimba kwa hisia wimbo wa kuisifia Tanzania mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza wakati wa uzinduzi wa Shindano la Kabati Star Search lilofanyika jana Mkoani Iringa.( Picha na Anitha Jonas -WHUSM)[/caption]Halikadhalika na mmoja wa washiriki wa mashindano hayo Yahya Hamadi alimshukuru mbunge huyo wa viti maalum kwa kuandaa mashindano hayo na ameahidi kuwa atajitahidi kufanya vizuri kwani anaamini kupitia jukwaa hilo nae anaweza kuja kuwa msanii maarufu katika Taifa.
Hata hivyo Naibu Waziri Shonza aliwasihi majaji wa mashindano hayo kutenda haki katika maamuzi wanayoyafanya kwani wao ndiyo wenye dhamana ya kutoa msanii atakayetangaza mkoa na taifa kwa ujumla katika ngazi za Kimataifa,ambapo mmoja wa majaji hao Bw.Roger Magoha kwa niaba ya wenzake aliahidi kusimamia hilo.