Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mwakalinga, Azitaka Taasisi za Ujenzi Kushirikiana
Feb 14, 2019
Na Msemaji Mkuu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, amezungumzia umuhimu wa taasisi zote zilizo chini ya Wizara yake kushirikiana ili kujengeana uwezo na uzoefu katika kusimamia na kutekeleza ujenzi wa miradi mikubwa kwa viwango na kasi.

Akizungumza na wataalam  wa Wakala wa Majengo nchini (TBA), Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na Vikosi vya Ujenzi vya Wizara hiyo mjini Dodoma  Arch. Mwakalinga, amesema ushirikiano huo ukifanikiwa utawezesha taasisi hizo kubadilishana uzoefu na utaalam katika kujenga na kusimamia miradi mingi mikubwa  kwa haraka na viwango bora na hivyo kuiongezea serikali mapato.

“Kuanzisa sasa hakikisheni  nyinyi TANROADS,TEMESA ,TBA,na VIKOSI vya UJENZI mnakutana mara kwa mara ili kujadiliana kwa pamoja na kupeana uzoefu utakaowezesha miradi ya ujenzi mnayoijenga na kuisimamia inakuwa na ushirikishwaji wa kitaalam na kiuzoefu ili kuwa na ubora na kuiwezesha kukamilika kwa wakati ”, amesema Arch. Mwakalinga.

Naye, Mkadiriaji Majenzi wa Wizara ya Ujenzi QS. Optatus Kanyesi, amemhakikishia Katibu Mkuu Mwakalinga kuwa ataratibu umoja huo wa Taasisi za sekta za ujenzi ili taasisi hizo ziwe na uwiano katika ubora wa huduma zake na kuleta tija kwa Serikali na jamii kwa ujumla.

Katibu Mkuu Mwakalinga, alikuwa katika ukaguzi wa miradi inayojengwa na kusimamiwa na taasisi zilizo chini ya sekta ya ujenzi ili kubaini changamoto na mahitaji ya miradi hiyo mjini Dodoma.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi