[caption id="attachment_40469" align="aligncenter" width="1000"] Madaktari Bingwa wa MOI kwa Kushirikiana na madaktari bingwa kutoka hospitali ya Zydus wakifanya upasuaji mgumu wa kupandikiza nyonga bandia katika vyumba vya upasuaji MOI[/caption] [caption id="attachment_40488" align="aligncenter" width="537"] Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) katika vyumba vya upasuaji MOI kwenye kambi ya upasuaji wa Nyonga na Mgongo inayofanywa kwa ushirikiano kati ya MOI na hospitali ya Zydus ya India[/caption]
Na Patrick Mvungi - MOI
Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kushirikianana hospitali ya Zydus ya nchini India kuanzia leo tarehe 14/02/2019 mpaka tarehe 16/02/2019 zitaendesha kambi maalum ya upandikizaji wa nyonga bandia na upasuaji wa Mgongo kwa njia ya kisasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amesema Katika kambi hii Madaktari bingwa wa MOI na Zdyus watashirikiana kufanya upasuaji mgumu wa kupandikiza Nyonga bandia pamoja na upasuaji wa mgongo kwa njia ya kisasa lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo madaktari bingwa wa MOI ambapo zaidi ya wagonjwa 6 watafanyiwa upasuaji.
“Huu ni muendelezo wa ushirikiano kati ya Taasisi yetu ya MOI na hospitali hii ya Zydus ya nchini Indi, awali tulishirikiana katika kliniki maalum na safari wamekuja kwenye kambi hii ya upasuaji, naamini madaktari Bingwa wetu watapata mbinu mpya na za kisasa ili waendelee kutoa huduma hizo hata baada ya wageni hawa kuondoka” Alisema Dkt Boniface
[caption id="attachment_40467" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Kimataifa wa hospitali ya Zydus bwana Himanshu Sharma akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) katika vyumba vya upasuaji MOI.[/caption]Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Uhusiano wa kimataifa wa hospitali ya Zydus Himanshu Sharma amesema ushirikiano kati ya MOI na Zydus umekuwa wenye mafanikio makubwa toka mwaka jana ambapo wagonjwa wamekuwa wakinufaika kwa kupata huduma kwa kutumia mbinu za kisasa bila ya kusafiri kwenda nje ya nchi.
“Tunafurahi kwamba tumepata fursa ya kuwapatia mbinu mpya na za kisasa za upasuaji wenzetu hapa MOI, teknolojia na mbinu za upasuaji zinabadilika kila siku na kwakuwa tunashirikiana, wataalamu wetu wameleta mbinu mpya ambazo tunazitumia kule India, lengo ni kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma kwa mbinu na teknolojia bora hapahapa Tanzania” alisema Bwana Sharma
[caption id="attachment_40465" align="aligncenter" width="1000"] Madaktari Bingwa wa MOI kwa Kushirikiana na madaktari bingwa kutoka hospitali ya Zydus wakifanya upasuaji wa mgongo kwa njia ya kisasa katika vyumba vya upasuaji MOI.[/caption]Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Mifupa wa MOI aliyebobea kwenye upandikizaji wa Nyonga bandia Dkt Violeth Lupondo amsema mbinu wanazopata zitawasadia kuendelea kutoa huduma hizo hata baada ya madaktari kutoka Zydus kuondoka.
“Huwa tunafanya kila siku aina hizi za upasuaji lakini huu wa leo ambao tunafanya na wenzetu kutoka Zydus ni wa tofauti na mgumu, tunajifunza mambo mengi kutoka kwao na wao pia wanajifunza kutoka kwetu, ni matarajio yetu wagonjwa wengi zaidi watanufaika” Alisema Dkt Lupondo
Hii ni sehemu ya Mkakati wa Taasisi ya MOI wa kuhakiklisha huduma zote za kibingwa zinapatikana hapa nchini na kwa teknolojia ya kisasa sawa na ile inayotumika kwenye mataifa yalioyoendelea.