[caption id="attachment_37768" align="aligncenter" width="900"] Mkurugenzi wa Ubora na Uhakiki wa Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia Wazee na Watoto Dr. Mohamed Mohamed akifungua kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]
Na Mwandishi Wetu; MOI
Mkurugenzi wa ubora na uhakiki wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Mohamed Mohamed leo tarehe 5/11/2018 amefungua kongamano la tano la kimataifa linalolenga kutoa mafunzo kwa madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu, mafunzo hayo yanafanyika kwa siku tano, siku mbili za nadharia na siku tatu za mafunzo ya vitendo ambayo itahusisha upasuaji.
Dkt Mohamed amesema kongamano hili la tano limehudhuriwa na zaidi ya madaktari 100 kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Ethiopia, Malawi, Namibia na nchi nyingine za Afrika, ulaya, na marekani ambapo mafunzo yatatolewa na Madaktari bingwa 8 wazalendo kutoka MOI na wengine 15 kutoka Marekani na Ulaya.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface amesema mafunzo haya yameratibiwa na Taasisi ya MOI kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Weil Cornel cha New York Marekani ambapo hii ni mara ya tano kufanyika hapa Tanzania (MOI).
“Mafunzo ya mwaka huu yatakuwa ya kipekee zaidi kwani wataalamu wetu watajifunza jinsi ya kufanya upasuaji wa kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo (Celebral aneurysm) kwa mara ya kwanza hapa nchini ,kabla ya hapo wagonjwa walilazimika kwenda nje ya nchi kwa gharama kubwa ” Alisema Dkt Boniface.
[caption id="attachment_37769" align="aligncenter" width="900"] Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya MOI Prof Charles Mkonyi akizungumza katika kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu linalofanyika Jijini Dar es Salaam.[/caption]Dkt Boniface amesema gharama za upasuaji huu nje ya nchi ni zaidi ya Tsh milioni 60 na hapa nchini haitazidi Tsh milioni 10 hivyo kuanza kwa huduma hii kutaokoa fedha nyingi za Serikali na tayari Serikali imeshanunua darubini maalum ya kufanyia upasuaji huu mkubwa.
Aidha, Dkt. Roger Hartl Mkurugenzi wa Kitivo cha upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu kutoka chuo kikuu cha Weill Cornell amesema ni heshma kubwa kufika Tanzania kwa mara nyingine, pia kupata fursa ya kubadilishana uzoefu na madaktari wa Tanzania na nchi nyingine duniani.
“Pamoja na mafunzo ya nadharia tutafanya upasuaji kwa pamoja kwa njia za kisasa, hili ndilo lengo letu hasa la kuja hapa, tunataka wenzetu wa MOI na madaktari walio mafunzoni waweze kutoa huduma hizo kwa weledi mkubwa, tumekuwa tukifanya hivi kwa muda sasa na tunaona wanakwenda vizuri hii inatia faraja sana” alisema Dkt Hartl.
[caption id="attachment_37770" align="aligncenter" width="817"] Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akitoa neno la ukaribisho katika kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu linalofanyika katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.[/caption]Pia, Dkt. Hartl amesema mafunzo ya mwaka huu yanalenga kuwajengea uwezo washiriki ili waweze kutumia teknoljia ya kisasa ya matibabu ya Ubongo na mgongo na kuwapa mbinu mpya za upasuaji hususani kwa mgonjwa aliyeumia kwenye eneo la mfumo wa fahamu hususani kwenye ubongo , uti wa Mgongo na mishipa ya fahamu iliyoharibika.
Taasisi ya MOI imeendelelea kufanya mageuzi makubwa katika huduma zake kwa lengo la kuhakikisha huduma zote za kibingwa zinapatikana hapa nchini na kuendelea kuokoa maisha ya watanzania na nchi nyingine za Afrika ambazo zinazoleta wagonjwa kutibibiwa MOI.
[caption id="attachment_37771" align="aligncenter" width="900"] Kiongozi wa jopo la wakufunzi kutoka chuo kikuu cha Weill Cornel cha marekani Prof Roger Hartl akiwasilisha mada katika kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo ,Mgongo na Mishipa ya fahamu linalofanyika katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_37772" align="aligncenter" width="900"]