Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waandishi Wahimizwa Kutangaza Fursa za Uwekezaji Mkutano wa SADC
Jun 12, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_44181" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi akizungumza katika Mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.Paramagamba Kabudi, Wahariri na Wamiliki wa Vyombo vya Habari, kuhusu Mkutano Mkuu Nchi wanachama wa Umoja wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ambapo Tanzania watakuwa Wenyeji Wa Mkutano huo mapema Mwezi Agosti 2019.[/caption]

Na: Mwandisi Wetu

Wakati Tanzania inajiandaa kupokea Mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwaAfrika (SADC) mapema Agost, vyombo vya habari vimekumbushwa umuhimu wa kuzibaini fursa za uwekezaji ili kuzitangaza kwa nchi zitakazoshiriki ili wawekezaji watakaofika nchini kuweza kuvutiwa kuwekeza nchini,

Mbali na mkutano huo wa SADC  utakaofanyika jijini Dar es Salaam Agost 17 -18. 2019 baada ya karibu miongo miwili, katika viwanja vya Mlimani City yatafanyika maonesho ya Wiki ya Viwanda Julai yatakayoanza  22-26,2019, ikiwa ni fursa ya kutambua nafasi ya viwanda katika nchi za SADC.

[caption id="attachment_44183" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.Paramagamba Kabudi, akisisitiza Jambo wakati wa Mkutano wake ,Wahariri, na wamiliki wa Vyombo vya Habari kuhusu Mkutano Mkuu Nchi Wanachama wa Umoja wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ambapo Tanzania watakuwa Wenyeji Wa Mkutano huo mapema Mwezi Agosti 2019.[/caption]

Akiongea na wamiliki wa vyombo vya habari na wahiriri, jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, amekumbusha wanahabari kutangaza dhima ya serikali ya kujenga viwanda, nafursa za kuwekeza katika kilimo, utalii na maeneo mengine.

Waziri amesema,”nafasi  yenu waandishi sio kuripoti tuma tukio katika siku za mkutano wa SADC, ni muhimu kushiriki katika hatua ya kuandaa, kushiriki mkutanoni na hata baada ya mkutano kushiriki tathmini ya hatua zote za vikao mbalimbali vya SADC na Mkutano Mkuu” amesisitiza

Pamoja na ajenda ya uwekezaji, Waziri huyo ambaye kiutumishi alianza na taaluma ya habari amewakumbusha waandishi juhudi za Tanzania baada ya Uhuru 1961 za mwalimu Nyerere alivyopigania Bara la Afrika, huku akizitaja nchi za Angola, Msumbiji, Afrika Kusini, Kenya, Rwanda na Burundi zilivyosaidiwa na Tanzania katika harakati zao zakujikomboa kutoka utawala wa wakoloni.

[caption id="attachment_44186" align="aligncenter" width="750"] Wahariri na Waandishi wakongwe wakifuatilia Mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.Paramagamba Kabudi, Wahariri na Wamiliki wa Vyombo vya Habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam leo, Kuhusu Mkutano Mkuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ambapo Tanzania watakuwa Wenyeji Wa Mkutano huo mapema Mwezi Agosti 2019.[/caption] [caption id="attachment_44187" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC, Dkt.Ayubu Rioba akifuatilia Mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.Paramagamba Kabudi, Wahariri na Wamiliki wa vyombo vya Habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam leo[/caption] [caption id="attachment_44188" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.Paramagamba Kabudi, Akizungumza katika Mkutano wake ,Wahariri, na wamiliki wa Vyombo vya Habari kuhusu Mkutano Mkuu Nchi Wanachama wa Umoja wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ambapo Tanzania watakuwa Wenyeji Wa Mkutano huo mapema Mwezi Agosti 2019, Kutoka kulia ni Katibu MOAT, Henry Mhanika, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Siasa na Utalii, Agnes Kayola, Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi.(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)[/caption]

“Vijana wengi wa kizazi cha sasa hawajui heshima kubwa inayostahili Tanzania kutokana na mchango wake kwa  nchi zinazotuzunguka … wanatakiwakujua, vyombo vya habari havielezei historia ya nchiyetu,” Waziri Kabudi amesema huku akiwasisitiza waandishi wakongwe kuwashirikisha waandishi vijana kujua yaliyofanywa na taifa lao baada ya Uhuru kukomboa nchi za kusini mwa Tanzania.

Nchi 16 za SADC zenye watuzaidi ya milioni 450 zina nafasi kubwa kunufaika na Tanzania kupata mali ghafi ya viwanda kutokana na nchi kuwa na nafasi kubwa ya ardhi ya rutuba ya kuweza kulima aina nyingi za mazao, pia ardhi yake kuwa na hifadhi ya maji mengi kwa kilimo na hifadhi za wanyama.

Waziri amesisitiza kwa  jamii ya watanzania kuona umuhimu wa mkutano huo, ambapo unakuja Tanzania tokea mwaka 2003, wakati nafasi ya Uenyekiti ulikuwa kwa Rais wa Tanzania (wakati huo), Benjamin Mkapa, kwa sasaRais wa NamibiandiyeMwenyekiti, baada ya kupokea toka Afrika Kusini na Makamu wake ni Rais wa Tanzania, Dkt John Magufuli atakabidhiwa nafasi ya uenyekiti Agost 18, 2019.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi