Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mkutano wa 23 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Mabadilko ya Tabianchi, Bonn, Ujerumani.
Nov 14, 2017
Na Msemaji Mkuu

 

  • Tanzania yasifiwa kwa uongozi bora na kasi kubwa ya maendeleo licha ya kukabiliwa na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Tanzania imetolewa mfano kama moja ya nchi zenye uchumi unaokuwa kwa kasi barani Afrika huku Rais wa Awamu ya Tano Mhe. Dr. John Pombe Magufuli akielezwa kama Rais wa mfano wa kuigwa kama Afrika inahitaji maendeleo ya kweli.

Haya yamesemwa na Bwana Cris Dodwell, msimamizi wa mradi wa kusaidia majiji,   katika uzinduzi wa mradi mkubwa wa kusaidia majiji makubwa tisa ya Afrika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ujulikanao kama “Cities Matter:   Capacity Building in Sub Saharan African  megacities  for transformational climate change action” unaofanyika mjini Bonn, Ujerumani.

Dar Es Salaam ni moja ya majiji tisa ambayo yameingizwa katika mradi huu unaofadhiliwa na serikali ya Ujerumani ambao umezinduliwa Bonn tarehe 13 Novemba, 2017. Majiji mengine ni Durban, Cape Town, Johannesburg na Tshwane- AfrikaKusini;  Addis Ababa; Nairobi; Lagos;  na Accra.  Dar Es Saalam imeingizwa katika mpango huu baada ya juhudi kubwa za Serikali ya awamu ya tano kuandaa miradi na kutafuta fedha za kusaidia kushughulikia changamoto za mabadiliko ya tabia nchi kwa kushirikiana na taasisi na mashirika mbalimbali duniani.

Uzinduzi huu umehudhuriwa na Mameya wa majiji yote haya pamoja na wataalamu wa mabadiliko ya tabia nchi kutoka nchi husika walioshiriki kuandaa mradi huu mkubwa kwa nchi za Afrika.  Meya wa jiji la Dar EsSalaam  Mhe. Isaya Mwita   Charles ameshiriki uzinduzi huu. Aidha, Mkurugezi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais  Bwana Richard Muyungi ameshiriki kwa upande wa Serikali. Pia wawakilishi wa Serikali ya Ujerumani na Meya wa jiji la Bonn wameshiriki .

Aidha wakati Mkutano huo ukiendelea mjini Bonn yamezinduliwa makumbusho maalum ya nchi na watu mashuhuri katika historia ya kushughulikia suala la mabadiliko ya tabia nchi kwa takribani miaka 50 iliyopita. Makumbusho haya yanajulikan kama “The Richard Kinley Gallery” yameanzishwa kwa kumbukumbu ya Bwana Richard Kinley aliyefanya kazi muda mwingi wa maisha yake katika eneo hili la mabadiliko ya tabianchi. Katika Makumbusho haya Tanzania imetajwa kati ya nchi ambazo zimetoa mchango mkubwa duniani katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi duniani hasa  pale ilipoongoza kwa umahiri mkubwa nchi za kundi la 77   (nchi zinazoendelea) wakati wa kupitisha mkataba wa Kyoto mwaka 1997 na wakati wakupitisha Makubaliano ya Paris mwaka 2015 ambao Tanzania iliongoza Marais wa Afrika chini ya Kamati Maalumu ya Marais kuhusu mabadiliko ya tabia nchi  ( CAHOSCC) kwa miaka miwili kwa mafanikio makubwa.

  Aidha, katika Makumbusho haya Bwana  Richard Muyungi, Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, amewekwa katika makumbusho haya akiwa ni miongoni mwa watu mashuhuri  49 duniani ambao wametoa mchango mkubwa duniani katika kukabiliana na mabadilko ya tabia nchi kwa kipindi cha takribani miaka 50 iliyopita.

Bwana Muyungi ameelezwa, pamoja na mambo mengine, kama mtaalamu mahiri na mpiganiaji wa haki za nchi maskini ambazo zinaathiriwa na athari za mabadiliko ya tabianchi kutokana na gesi joto zinazosababishwa na nchi tajiri; na hasa yeye kama mwasisi na mwanzilishi wa mfuko wa nchi maskini duniani wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi mwaka 2001 “Least Developed Countries Fund - LDCF” na Mfuko wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi (Adaptation Fund – AF)  ambayo hadi sasa imesaidia mamilioni ya wananchi maskini duniani kote.

Mifuko hii hadi sasa imetoa zaidi ya USD 1.5 billion kwa Wananchi zaidi ya milioni 500 katika Nchi maskini duniani kote na Nchi zinazoendelea.  Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimenufaika na uwepo wa Mifuko hii kupitia miradi  katika Ofsisi ya Makamu wa Rais, ya ujenzi wa ukuta wa bahari wa Pangani (Tanga), Kilimani na KisiwaPanza (Zanzibar) na uchimbaji wa visima Bagamoyo (Pwani) na mradi wa Kujenga Ukuta wa bahari Barabara ya Obama na Kigamboni na ujenzi wa mitaro,  Buguruni (Ilala) na Miburuni (Temeke).

   

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi