[caption id="attachment_10063" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bibi Maimuna Tarishi akifungua mkutano wa siku moja wa wadau kuchangia utekelezaji wa mkakati wa Kitaifa wa miaka mitano wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto mapema hii leo jijini Dar es Salaam.[/caption]
Na: Anthony Ishengoma, MAENDELEO YA JAMII
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto inatafsiri kwa Kiswahili Mkakati wa Taifa wa miaka mitano wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ili kurahisisha mawasiliano kwa kuanzia ngazi ya Taifa hadi Kijiji.
Hayo yamebainika Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Sihaba Nkinga, wakati wa Kikao kazi na wadau wa Maendeleo kuchangia fedha za utekelezaji wa Mkakati huo.
[caption id="attachment_10076" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Anna Maembe akifafanua jambo wakati wa mkutano wa siku moja wa wadau kuchangia utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa miaka mitano wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]Mkakati huo unatafsiriwa ili kutatua changamoto ya mawasiliano iliyopo katika utekelezaji wake kuanzia ngazi za chini hadi juu Kitaifa ili kurahisisha utekelezaji wake ikiwa ni namna mojawapo ya kuimarisha na kutafuta namna bora ya kurahisisha mawasiliano katika ngazi zote.
Mkutano huo na wadau wa maendeleo unalenga kutafuta fedha takribani Tsh. bilioni 250 za Tanzania zitakazo tolewa na Serikali pamoja na wadau wa maendeleo ili kuwezesha utekelezaji wa Mkakati huo Nchini kote.
[caption id="attachment_10074" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Mipango toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Atupele Mwambene akitoa mada wakati wa mkutano wa siku moja wa wadau kuchangia utekelezaji wa mkakati wa Kitaifa wa miaka mitano wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Wakati huohuo Katibu Mkuu Ofisi ya Wiziri Mkuu Maimuna Tarishi wakati wa kutoa salamu za ufunguzi wa kikao kazi hicho amesema mchakato wa utengenezaji wa Mkakati huo ulizingatia sana malengo ya millennia ya 2030 na Malengo ya Agenda 2063 ya Tume ya Umoja wa Afrika na kusisitiza kuwa kinachotakiwa sasa ni kutafuta namna bora ya utekelezaji wa Mkakati huo.
Tanzania ni moja ya Nchi nne Duniani na ya kwanza Afrika kupewa nafasi ya mfano kuwa katika nafasi nzuri ya kutokomeza vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto kwa sababu ya mchango wake katika tafiti zinazohusiahana na masuala ya ukatili.