Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Milango ya Uwekezaji TCAA ipo wazi - Prof. Mbarawa.
Sep 19, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_14467" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari akifafanua jambo kwa washiriki wa Mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa wadau wa usafiri wa anga mapema hii leo jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na. Neema Mathias na Thobias Robert.

Serikali imesema kuwa, ipo tayari kufanya kazi na sekta binafsi na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi katika kuendeleza na kujenga miundombinu bora ya usafiri wa anga ili kufikia sera yake ya uchumi wa kati ifikapo 2025.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa alipokuwa akizungumza na wadau wa sekta ya usafiri wa anga hapa nchini katika jukwaa liliondaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa anga (TCAA) litakalofanyika kwa siku mbili kwa lengo la kujadili  mikakati  na changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

 “Hii ni biashara, hivyo tunataka kuinua sekta ya usafiri wa anga kwa maendeleo bora ya Waafrika,  msilete wawekezaji ambao hawana mikakati ya kuinua sekta hii, badala yake leteni wawekezaji wenye uchache wa maneno na wingi wa vitendo milango ipo wazi na sisi tupo tayari,” alifafanua Prof. Mbarawa.

[caption id="attachment_14468" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Leonard Chamuriho akizungumza na washiriki wa Mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa wadau wa usafiri wa anga mapema hii leo jijini Dar es Salaam.[/caption]

Prof. Mbarawa amesema kuwa katika mpango wa nchi yetu kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025, ni lazima tujenge miundombinu ya kisasa ambayo huanzia kwenye reli, meli, barabara na usafiri wa anga. Serikali imeamua kuungana na wadau wa sekta hii katika kujadili changamoto ya uhaba wa Marubani, Wahandisi wa ndege, uchukuzi wa mashehena ikiwa ni pamoja na utatuzi wake.

“Usafiri wa anga ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa taifa letu kwani kupitia usafiri huo tunaweza kuongeza  idadi ya watalii, ajira, na  fedha za kigeni pamoja na kuchangia ukuaji wa sekta nyingine,” alisema Prof Mbarawa.

Aliongeza kusema kuwa, ni jambo la kushangaza kuona leo samaki wanaovuliwa mkoani Mwanza wanasafirishwa nje ya nchi kupitia kiwanja cha ndege cha Entebbe kilichopo  nchini Uganda na siyo kiwanja kilichopo Mwanza, pia maua yanayolimwa mkoani Arusha yanasafirishwa nje ya nchi kupitia Nairobi na siyo uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro.

Prof. Mbarawa amewasisitiza TCAA na wadau kuhakikisha kuwa wanajadili kwa kina namna ya kuzikabili changamoto hizo na kutoka na majibu kamili yatakayoiwezesha serikali  kujua namna ya kushirikiana nao katika kuziondoa.

[caption id="attachment_14469" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akisisitiza jambo kwa washiriki wa mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa wadau wa usafiri wa anga nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_14470" align="aligncenter" width="750"] Baadhi wa washiriki wa mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa usafiri wa anga nchini wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. makame Mbarawa wakati wa uzinduzi wa mkutano huo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa.[/caption]

Aidha

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Anga, Hamza Johari   amesema kuwa lengo kubwa ni kujipanga katika kuelekea dira ya uchumi wa kati, hivyo kupitia jukwaa hilo ambalo litakuwa likifanyika  mara mbili kwa mwaka wataendelea kuwashirika wadau namana ya  kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili.

“Lengo la jukwaa hili ni kujitathimini upya kwani kusafirishwa kwa shehena kupitia viwanja vya wenzetu inaonesha kuwa sisi tuna tatizo, haileti tija kuwa na bidhaa zetu zinazonufaisha nchi za jirani,” alifafanua Johari.

Aidha Johari alieleza kuwa, TCAA inataka kuufanya  Uwanja wa Julius Nyerere kuwa kituo kikuu kama ilivyo uwanja wa Dubai ili kuvutia abiria wengi zaidi katika kutumia viwanja vyetu.

Aliendelea kusema kuwa, jukwaa hilo linalenga kujadili namna ya kuzitumia sekta binafsi  katika kujenga miundombinu ya usafiri wa anga hapa nchini pasipo kuitegemea serikali pekee yake kama inavyoanisha sera ya kushirikisha sekta binafsi ya mwaka 2010 katika kuendeleza miundombinu ya viwanja vingine vya ndege ambavyo havifikiki vizuri.

“Malengo yetu baada ya jukwaa hili ni kuwa na mpango mkakati unaopimika ambao tutaupleleka kwa serikali kuu ili wauone na baada ya hapo tutaanza utekelezaji, Tanzania ya viwanda 2025 inawezekana,” aliongeza Johari.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi