[caption id="attachment_44435" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akihutubia wananchi na baadhi ya viongozi wa Serikali, kwenye Kongamano la nne la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Juni 15.2019. (PichanaOfisiyaWaziriMkuu).[/caption]
Na Frank Mvungi- Dodoma
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameiagiza Mikoa na Halmashauri zote Nchini kuanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili kuendana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano kukuza uchumi kupitia uwezeshaji.
Akizungumza Jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la nne la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi linaloratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Mhe. Majaliwa amesema kuwa kuanzishwa kwa vituo hivyo kutasaidia kuwawezesha wananchi na kukuza biashara akitolea mfano kituo cha Uwezeshaji wananchi kiuchumi katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga ambacho kimeonesha mafanikio makubwa.
"Wafanyabishara kutoka Kigali Rwanda na Bujumbura Burundi na maeneo mewngine wanafika Kahama kufanya manunuzi yao kutokana na kukua kwa biashara katika eneo hilo kwa sababu ya kuwepo kwa kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi’’ Alisisitiza Mhe. Majaliwa.
Akifafanua amesema kuwa Tozo Zaidi ya 54 zimefutwa na Serikali ikiwa ni moja ya hatua za kuondoa vikwazo vya kibiashara hali inayoweka mazingira bora kwa wafanyabiashara kukuza na kuendeleza biashara zao.
Alibainisha kuwa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi linao uwezo mkubwa wa kusimamia miradi ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.
[caption id="attachment_44434" align="aligncenter" width="750"]Pia alizielekeza Mamlaka za Serikali kuhakikisha kuwa zinashirikiana na wadau katika kutekeleza sera na mipango yote katika kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Aliongeza kuwa Serikali imeendelea kuondoa vikwazo katika biashara kwa kukutana na wafanyabiashra na kuwapa fursa ya kubainisha changamaoto zao ili Serikali iweze kuchukua hatua stahiki katika kuzitatua lengo likiwa kuendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji hapa nchini.
“ Mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa , Singida na Shinyanga kukamilisha muongozo wa uwekezaji katika kipindi cha mwaka mmoja” Alisisitiza Mhe MajaliwaAlitaja baadhi ya hatua zilizochukuliwa katika kuwezesha wananchi Mhe. Majaliwa amesema kuwa ni pamoja na kutungwa kwa sheria ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2018 lengo likiwa kuwezesha wananchi kujikwamua kiuchumi.
“Serikali inatekeleza sera ya Taifa ya uwezeshaji ya mwaka 2004 na sheria yake, lengo likiwa kuweka mazingira ya uwezeshaji wananchi kiuchumi”. Alisisitiza Mhe Majaliwa
Pia alilihakikishia Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP) kuwa Serikali itaendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi yote inayolenga kuwawezesha wananchi kiuchuni.
[caption id="attachment_44433" align="aligncenter" width="750"]“Endeleeni kuratibu masuala yote ya uwezeshaji wananchi ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi inayoelekeza uwezeshaji wa wananchi husasani uanzishwaji wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa ili kukuza uchumi na ustawi wa wananchi wetu”. Alieleza Mhe Majaliwa
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Kongamano la uwezeshaji wananchi kiuchumi linafanyika kila mwaka ili kutoa fursa kwa wadau kukaa pamoja na Serikali kubainisha changamoto na kutoa mapendekezo ya namna ya kuzitatua.
Aliongeza kuwa Kongamano hilo limeshirikisha wadau kutoka sekta umma, binafsi, wadau wa maendeleo,Taasisi za elimu na Taasisi za Kijamii.
[caption id="attachment_44432" align="aligncenter" width="750"]Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezshaji Wananchi Kiuchumi Bi Beng’ Issa amesema kuwa jitihada za makusudi zimeendelea kufanyika ili kuwawezesha wananchi kwa lengo la kuongeza ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji kupitia sekta ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Aliongeza kuwa Hati za Hakimiliki ya ardhi na hati ya Kimila zimewezesha wamiliki wa ardhi kuzitumia hati hizo kama dhamana ya mikopo katika taasisi za fedha.
“ Katika kipindi hiki, Hati za hakimiliki 32,526 zimetolewa, Aidha, Hati za Hakimiliki za Kimila 88,840 zimetolewa kupitia programu ya kuwezesha Umilikishaji Ardhi inayotekelezwa katika Wilaya za Malinyi, Ulanga na Kilombero” Alisisitiza Bi Beng’.
Akizungumzia mafanikio mengine katika uwezeshaji wananchi Bi Beng amesema kuwa ni pamoja na ushiriki wao kwenye miradi ya kimkakati ikiwemo kuzingatiwa kwa ununuzi wa huduma na bidhaa kutoka katika Kampuni za kitanzania kuanzia Julai 2018 hadi Machi 2019 kumekuwa na mafanikio mengi ikiwemo;
Wanachi wengi walijipatia ajira katika ujenzi wa mji wa Serikali Ihumwa kutokana na ujenzi wa mji huo na pia malighafi zilizotumika katika ujenzi wa majengo ya Wizara zimetokana na viwanda vya hapa nchini na hivyo kuongeza kasi ya uwekezaji wa ndani.
Hata huduma mbalimbali za utoaji wa vifaa vya Ofisini zilitolewa na kamapuni za kitanzania zilizosajiliwa na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini ambazo hupatikana kwa ushindani baada ya zabuni kutangazwa.
Hata ushiriki wa wananchi katika miradi mikubwa kama ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango cha Kimataifa na miradi mingine mingi ni chachu ya maendeleo kwa kuwa wameweza kupatan najira na kuuza huduma mbalimbali kwa makampuni yanayojenga miradi hiyo.
Kongamano la uwezeshaji wananchi kiuchumi limefanyika Jijini Dodoma na kuwashirikisha wadau mbalimbali, viongozi wa Serikali wakiwemo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala, Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Kimataifa.