[caption id="attachment_40538" align="aligncenter" width="900"]
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akioneshwa mtindo wa paa kwa ndani utakavyokuwa katika jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii na Mkandarasi Clement Shaibu wakati alipotembelea kwa ajili ya kukagua jengo hilo linalojengwa Ihumwa jijini Dodoma[/caption]
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ametaka ujenzi wa majengo ya Wizara mbalimbali yanayojengwa katika eneo la Ihumwa yajikite kutumia vyuma badala ya kutumia mbao ngumu ambapo kwa sasa Wizara ipo kwenye kampeni kubwa ya kuzuia matumizi ya miti hiyo ambayo ipo hatarini kutoweka
Amesema Wizara kwa sasa imepiga marufuku ukataji na usafirishaji wa magogo yanayozalisha mbao ngumu.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri huyo wakati alipotembelea eneo hilo kwa ajili ya kukagua hatua za ujenzi wa jengo hilo unaoendelea jijini Dodoma.
Amesema endapo majengo ya Wizara zote yatatumia mbao za aina hizo zaidi ya magogo ya miti 300 itakatwa.
Aidha, Mhe.Kanyasu ameshauri Jengo la Wizara hiyo lisitumie nguzo za mbao kwa upande wa mbele katika sehemu ya kuingilia kama inavyoonekana kwenye ramani badala yake itumie nguzo za zege ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
[caption id="attachment_40539" align="aligncenter" width="900"]
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii (katikati) akiwa na Mkandarasi pamoja na Katibu wake, Zulu Ngondya (kulia) wakiangalia baadhi ya ramani ya jengo la Wizara hiyo mara baada itakapokamilik[/caption]
Pia, Mhe.Constantine Kanyasu ametaka timu ya wataalam mbalimbali ifanye kazi kwa pamoja katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa jengo hilo la Wizara katika mji wa Kiserikali wa Ihumwa.
Amesema licha ya kuwa hatua ya ujenzi wa jengo hilo ni ya kuridhisha ila ametaka nguvu ziongezwe ili kuweza kulikamilisha jengo hilo ndani ya muda wa wiki mbili zijazo licha ya kuwa muda uliotolewa na Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa tayari umeshapita.
Katika nyingine, Mhe Kanyasu ameshauri hatua za kupanda miti pamoja kuandaa bustani za maua zianze mapema katika jengo hilo ili likishakamilika liwe kwenye madhari nzuri badala ya kusubili hadi pale jengo litakapokamilika kabisa
Kwa upande wake, Mkandarasi wa Suma JKT, Clement Shaibu amemueleza Naibu huyo kuwa ujenzi unaendelea vizuri na wanatarajia kukamilisha ndani ya wiki mbili zijazo.