Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mfumko wa Bei za Bidhaa Wazidi Kupungua Hapa Nchini
Sep 08, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na: Thobias Robert

Mfumko wa bei za bidhaa za vyakula na sizizo za vyakula umepungua hapa nchini kwa mwezi Augusti kwa asilimia 5 ikilinganishwa na  mwezi Julai ambao ulikuwa ni asimilia 5.2, huku Fahirisi za bei zikipungua hadi 108.46 ikilinganishwa na mwezi Julai ambayo ilikuwa ni 108.85.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Bw. Ephraim Kwisegabo katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika ofisi ya Taifa ya Takwimu ikiwa ni lengo la ofisi hiyo kuijulisha jamii juu ya mfumko wa bei kwa bidhaa za vyakula na nishati hapa nchini.

“Kupungua kwa Fahirisi za bei kwa mwezi August kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei za baadhi ya vyakula hapa nchini pamoja na baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula kama vile diesel pamoja na petrol,” alifafanua Bw. Kwisegabo.

Aidha Bw. Kwisegabo, alivitaja baadhi ya Vyakula vilivyoshuka bei kwa mwezi August ni pamoja na Mchele kwa asilimia 1.2, mahindi 1.2, unga wa mahindi 1.6, dagaa 3.4, mbogamboga 1.2, maharage 3.2 viazi 3.5, pamoja na ndizi za kupika 2.4.

Vilevile Bw. Kwisegabo alizitaja baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kushuka kwa mfumko wa bei kuwa ni dizeli kwa asilimia 2.2, petrol asilimia 2.4 pamoja na vifaa vya kielektroniki kwa asimilia 1.6. lakini pia aliongeza kuwa mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani umepungua kwa mwezi August hadi asilimia 9.1 kutoka asilimia 9.3 kwa mwezi Julai.

Mbali na hayo, Bw. Kwisegabo alisema kuwa thamani ya shilingi 100 ya Tanzania imeongezeka ikilinganishwa na mwezi uliopita ambapo alisema, “uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 92.20 mwezi August, ikilinganishwa na shilingi 91.87 ilivyokuwa mwezi Julai ya mwaka huu.”

Bw. Kwisegabo, alisema kuwa, mfumuko huo umepungua zaidi ikilinganishwa na nchi ya Kenya, ambapo mfumko huo umeongeza kwa asilimia 8.04 ikilinganishwa na mwezi Julai ambao ulikuwa asilimia 7.47, kwa upande wa Uganda mfumko wa bei umepungua sawa na Tanzania ikiwa ni asilimia 5 ikilinganishwa na 5.2 kwa mwezi August.

Ofisi ya Sensa na Takwimu za Jamii imekuwa na utaratibu wa kutoa takwimu hizo kila mwisho wa mwezi hapa nchini ili kuijulisha jamii hususai juu ya kupanda au kushuka kwa mfumuko wa bidhaa za vyakula na sisizo za vyakula.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi