Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akieleza azma ya Serikali kuendelea kusimamia mashirika yote iliyowekeza ili yatoe gawio kwa Serikali hali itakayochochea maendeleo zaidi kwa wananchi kama ilivyo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano, hayo yamejiri wakati wa hafla ya kupokea gawio la shilingi Bil.15.2. Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna akizungumza wakati wa hafla ya Benki hiyo kukabidhi mfano wa hundi ya gawio kwa Serikali ya shilingi Bil.15.2 kwa Serikali kwa kipindi cha mwaka 2019 leo Agosti 19, Jijini Dodoma. Msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbuttuka akizungumzia mafanikio ya ofisi hiyo kwa kipindi cha Serikali ya Awamu ya Tano leo Agosti 19, Jijini Dodoma wakati Benki ya NMB ikiwasilisha gawio kwa Serikali. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dkt. Edwin Mhede akitoa maelezo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati wa hafla ya Benki hiyo kukabidhi gawio kwa Serikali leo Agosti 19, 2020 Jijini Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akifurahia mfano wa hundi ya gawio kutoka Benki ya NMB leo Jijini Dodoma ambapo Benki hiyo imetoa gawio la kiasi cha shilingi Bil. 15.2 kwa Serikali kwa kipindi cha mwaka 2019. Sehemu ya watendaji wa Benki ya NMB wakifuatilia hafla ya Benki yao kuwasilisha gawio kwa Serikali leo Agosti 19, 2020 Jijini Dodoma. Sehemu ya watendaji wa Ofisi ya Msajili wa Hazina wakifuatilia hafla ya Benki ya NMB kuwasilisha gawio kwa Serikali leo Agosti 19, 2020 Jijini Dodoma.
Giza
Mwanga
Chaguo Msingi
Ndogo
Kawaida
Kubwa