[caption id="attachment_52260" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe (aliyevaa kofia) alikagua mtambo wa kukoboa mpunga wa katika mradi wa ghala la kijiji cha Mvumi kilichopo wilayani Kilosa. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya.[/caption]
Na Mwandishi Wetu
Makatibu Wakuu wa Wizara nne leo wamefanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji mkoani Morogoro na kuridhishwa na kukamilika kwa ghala la kuhifadhia lililopo mpunga kijiji cha Mvumi Wilaya ya Kilosa.
Ziara hii imewashirikisha Makatibu Wakuu wa Wizara za Kilimo, Gerald Kusaya, Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe, Naibu Katibu Mkuu OR -TAMISEMI Bw. Gerlad Mweli na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais ,Mazingira, Balozi Joseph Sokoine.
Akizungumza kwenye ukaguzi huo, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya alisema ghala la kijiji cha Mvumi limekamilika na muda si mrefu litakabidhiwa kwa wakulima ili litumike.
[caption id="attachment_52261" align="aligncenter" width="750"]Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Gerlad Mweli amewataka wanakijiji wa Mvumi kujitolea kukamilisha ujenzi wa uzio wa ghala hilo ili kuimarisha ulinzi. ameshauri utaratibu uwekwe kwa kila mkulima atakayetunza mazao yake ghalani kuchangia fedha kidogo kwa ajili ya ujenzi wa uzio.
Naye mkulima James Nkalalwe wa kijiji hicho ameishukuru Serikali kwa kukamilisha mradi huo kwa sababu wanatarajia mradi huo utawaongezea tija na uchumi wa wakulima.