Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Awataka Wanawake Kuchangamkia Fursa ya Majukwaa ya Kiuchumi.
Aug 26, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_10424" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akisisitiza jambo kwa kina mama (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi kwa Kinamama Mkoa wa Dar es Salaam katika viwanja vya TTCL Kijitonyama leo. (Picha na: Eliphace Marwa.)[/caption]

Na: Ismail Ngayonga,

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka wanawake nchini kuchangamkia fursa ya uanzishaji wa majukwaa ya kiuchumi ili waweze kuunganisha nguvu katika upatikanaji wa masoko, mitaji, na elimu ya ujasiriamali hatua itakayowasaidia kupiga hatua kubwa na haraka za maendeleo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kuwezesha Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Dar es Salaam leo (Agosti 26, 2017) Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais amesema siri kubwa ya kuinua hali za kiuchumi kwa mwanamke, ni wanawake wenyewe kuweka nguvu za kufikiri na mipango thabiti.

[caption id="attachment_10426" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi kwa Kinamama Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Sophia Mjema akisisitiza jambo kwa kina mama (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa hilo iliyofanyika katika viwanja vya TTCL Kijitonyama leo.[/caption]

Aliongeza kuwa muda umefika wa kuwakukomboa wanawake kutoka katika lindi la umaskini linalotokana na kutowezeshwa kiuchumi, na hilo litawezekana kwa kuwapa ujuzi na maarifa, kuwawezesha kupata mikopo yenye riba nafuu na kwa urahisi pamoja na kuweka mifumo ya kisheria itayopiga vita mila kandamizi.

“Nimefarijika kusikia kuwa mpaka leo hii ukijumuisha na jukwaa hili la Dar es Salaam tuna majukwaa 23 ya Mikoa, 105 ya Halmashauri, 236 ya Kata, nitoe rai kwa mikoa ya Dodoma, Njombe na Ruvuma kuhakikisha kuwa inaanzisha haraka majukwaa hayo” amesema Mhe. Samia.

Aidha Makamu wa Rais alisisitiza kuwa ni vyema uwepo utaratibu wa kutembelea majukwaa hayo ili kuweza kubadilishana uzoefu sambamba na kusambaza fursa zinazojitokeza katika majukwaa ya vijijini ili kuhakikisha kuwa kila mwanamke Mtanzania ananufaika na keki ya taifa.

[caption id="attachment_10427" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu akikata utepe wa mfano wa hundi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi kwa Kinamama Mkoa wa Dar es Salaam katika viwanja vya TTCL Kijitonyama leo.[/caption] [caption id="attachment_10432" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu (kushoto) akipokea hundi toka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi kwa Kinamama Mkoa wa Dar es Salaam iliyofanyika katika viwanja vya TTCL Kijitonyama leo.[/caption]

Kwa mujibu wa Mh Samia, ajenda mpya ya malengo ya maendeleo endelevu imeazimia kukamilisha yote yaliyokuwa hayajatekelezwa katika malengo ya maendeleo ya millennia na kuhakikisha kuwa ifikapo ukomo wa utekelezaji wa ajenda ya malengo ya maendeleo endelevu mwaka 2030, usawa wa mwanamke utakuwa umefikia asilimia 50 kwa 50.

Katika hotuba yake hiyo Mhe. Samia alitoa wito kwa washiriki kulitumia vyema jukwaa hilo ili waweze kujipanga na kujikomboa kiuchumi kwa kuhakikisha wanaijenga Tanzania mpya ya viwanda kwa kujishughulisha na uzalishaji wa mazao ya kilimo ambayo ndio malighafi kuu ya kuendesha viwanda hivyo.

“Muda umefika sasa wa kuhakikisha kuwa hamtambuliki tu kwa ‘mwanamke jiko’ bali mwanamke ‘viwanda’, hapa namaanisha mwanamke mwenye maamuzi yake kiuchumi, kielimu, kibiashara, kisiasa na mwenye uwezo wa kushika nyadhifa mbalimbali” amesema Makamu wa Rais.

[caption id="attachment_10433" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu (katikati) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni ishirini kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi kwa Kinamama Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Sophia Mjema (kushoto) na kulia ni Mwenekiti wa Baraza la Wafanyabiashara Wanawake Bi. Jackline Maleko, mapema hii leo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi kwa Kinamama Mkoa wa Dar es Salaam .[/caption]

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei amebainisha kuwa kati ya asilimia 17 ya watanzania wanaotumia huduma rasmi za kibenki, wanawake ambao ni asilimia 52 ya watanzania milioni 56 wanaotumia huduma rasmi ya kibenki ni asilimia 10.1 tu kati ya watanzania wanaotumia huduma za kibenki.

Dkt. Kimei anasema kupitia jukwaa, hilo Benki hiyo imeweza kuzindua rasmi huduma ijulikanayo SIMAccount, ambayo inatoa fursa kwa wateja kuwa na uwezo wa kufungua akaunti za vikundi, hatua ambayo itaweza kutoa suluhisho la utunzaji wa fedha kwa wanawake na wanaume ikiwemo kuangalia miamala na kumbukumbu.

“Kupitia huduma ya SIMAccount, kinamama watakuwa na uwezo wa kufungua akaunti ya kikundi na kuwaunganisha wenzao mtandaoni bila ulazima wa kukutana, kama yalivyo makundi maarufu ya What’sup” amesema Dkt. Kimei.

[caption id="attachment_10435" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya kina mama wakifurahia jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi kwa Kinamama Mkoa wa Dar es Salaam iliyofanyika katika viwanja vya TTCL Kijitonyama leo. (Picha na: Eliphace Marwa.)[/caption]

Kwa mujibu wa Dkt. Kimei kwa wateja wapya ambao simu zao bado hazipo katika mfumo, watatakiwa kukamilisha usajili wao kupitia tawi la benki hiyo au kupitia wakala wa fahari huduma ambao kwa sasa wapo zaidi ya 2,500 nchi nzima.

Alisisitiza kuwa huduma hiyo ya SIMAccount itakuwa suluhisho la kipekee kwa wanawake na Watanzania kwa ujumla kwa kuwa itawezesha kufungua akaunti zao za vikundi pale walipo, kujiunga wenyewe na kutengeneza miundombinu ya kukopeshana wenyewe.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi