Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Majaliwa Kufungua Mkutano wa Mawaziri SADC kwa Njia ya Video
Mar 10, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_51524" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Kanali Wilbert Ibuge akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Mabadiliko ya mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakao fanyika kwa njia ya Mfumo wa Video kufuatia mripuko wa ugonjwa wa Corona (CODIV-19) ambao kwa sasa umeikumba nchi ya Afrika ya Kusini ambayo pia ni Nchi mwananchama wa Jumuiya ya SADC.[/caption]

Na Erick Msuya

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Kanali Wilbert Ibuge katika kituo cha mikutano Mwalimu Nyerere (JNICC) baada ya kutoa taarifa fupi ya kikao cha dharura cha Mawaziri wa SADC sekta ya Afya kilichojadili hali halisi ya Ugonjwa wa Corona  (CODIV- 19)  katika Nchi za SADC.

Amesema Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na kuendeshwa kwa  njia ya mfumo wa  Video (Video Conference) kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Corona (CODIV-19) ulioikumba nchi ya Afrika ya Kusini ambayo pia ni Nchi mwananchama wa Jumuiya ya SADC.

[caption id="attachment_51525" align="aligncenter" width="750"] Naibu Katibu Mtendaji wa Maswala ya Ushirikiano wa Kikanda (SADC) Thembinkosi Mhlongo akifafanua ajenda ya Mfumo mpya wa Hati ya Kusafiria za SADC itakayojadiliwa katika mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Nchi wanachama wa jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wanaoshughulikia Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Fedha Uchumi pamoja na viwanda na Biashara.[/caption]

“Kufatia Ushauri uliotolewa katika maazimio ya kikao cha Mawaziri wa  Afya wa SADC, kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC sasa hivi kitafanyika kwa njia ya video  tofauti na ilivyozoeleka, hivyo kila Nchi mwanachama wa SADC atakuwa nchini kwake huku tukijadili kwa njia ya video” alisema Balozi Ibuge.

Kwa upande wake  Naibu Katibu Mtendaji wa Maswala ya Ushirikiano wa Kikanda (SADC) Thembinkosi Mhlongo amesema kuna haja ya Nchi wanachama wa SADC kutumia hati ya kusafiria (Pasport) inayoweza kukumruhusu kila Mwanachama kusafiri na kufanya Shughuli za maendelo katika umoja wa SADC bila bugudha.

  [caption id="attachment_51527" align="aligncenter" width="750"] . Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Kanali Wilbert Ibuge akizungumza na waandishi wa habari juu ya Mabadiliko ya mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakao fanyika kwa njia ya Mfumo wa Video kufuatia mripuko wa ugonjwa wa Corona (CODIV-19) ulioikumba nchi ya Afrika ya Kusini ambayo pia ni Nchi mwananchama wa Jumuiya ya SADC.[/caption]

“Umoja wa Mataifa na jumuiya nyingine mengine wana Hati zao za kusafiria, na sisi tunahaja ya kuwa na hati zetu za kusafiria tukiwa kama SADC, katika jumuiya yetu kuna watu watafanyakazi kwa muingiliano wa kikanda hivyo ni muhimu kutumia hati moja” Alisema Mhlongo.

[caption id="attachment_51528" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Kanali Wilbert Ibuge (wapili kutoka kushoto aliyevaa koti rangi Nyeusi) akiwa na wajumbe wengine wa SADC mara baada ya kuwasili katika mkutano na waandishi wa habari juu ya Mabadiliko ya mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakao fanyika kwa njia ya Mfumo wa Video kufuatia mripuko wa ugonjwa wa Corona (CODIV-19) ulioikumba nchi ya Afrika ya Kusini ambayo pia ni Nchi mwananchama wa Jumuiya ya SADC.[/caption]

Miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa katika mkutano huo ni mazingira wezeshi ya maendeleo ya viwanda, masuala ya fedha na Michango ya Jumuiya, hati za kusafiria za SADC, na uanzishwaji wa shirika la utalii kwa nchi za kusini mwa Afrika.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi