Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ameshika mawe yenye madini ya Bati wakati alipokagua mitambo ya kampuni ya kuchenjua madini ya Bati ya African Top Minerals iliyopo Kyerwa Mkoani Kagera, Septemba 20 2021. Kulia ni Mhasibu wa Kampuni hiyo, Hamisi Kohomin
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakipata maelezo kuhusu madini ya Bati kutoka kwa Hamisi Kohomin ambaye ni Mhasibu wa Kampuni ya Kuchenjua Madini ya African Top Minerals ya Kyerwa Mkoani Kagera wakati Waziri Mkuu alipokagua mitambo ya kampuni hiyo, Septemba 20, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakishuhudia wakati Hamis Kohomin ambaye ni Mhasibu wa kampuni ya kuchenjua madini ya Bati ya African Top Minerals ya wilayani Kyerwa akiwaonesha namna ya kupima ubora wa madini hayo, Septemba 20, 2021. Mheshimiwa Majaliwa yuko Mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na viongozi wa kampuni ya kuchenjua mkadini ya Bati (TIN) ya African Top Minerals baada ya Waziri Mkuu kukagua mitambo ya kampuni hiyo wilayani Kyerwa, Kagera, Septemba 20, 2021. Wa tano kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali, Charles Mbuge.