Kibanda cha Mlinzi kilichopo kwenye lango kuu la kuingia katika ofisi ya TANESCO ya Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ambacho kimejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 7.03. Mhe. Majaliwa alikataa kufungua ofisi hiyo kama livyopangwa kwenye ratiba ya ziara yake mkoani Kagera, Septemba 20, 2021 baada ya kubaini kuwa limejengwa kwa gharama kubwa
.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na akizungumza na wafanyakazi wa TANESCO, Ofisi ya Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera kabla hajakataa kuifungua ofisi hiyo kama alivyopangiwa kwenye ratiba ya ziara yake mkoani Kagera baada ya kubaini kuwa gharama zilizotumika kujenga ofisi hiyo ni kubwa. Wa pili kulia ni Mkewe, Mary Majaliwa na kulia ni Meneja Mwandamizi Usambazaji wa TANESCO, Mhandisi Natthanasias Nangali .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza taarifa ya ujenzi wa ofisi ya TANESCO Wilaya ya Kyerwa iliyokuwa ikisomwa na Meneja Mwandamizi Usambazaji wa TANESCO, Mhandisi Natthanasias Nangali (wa tatu kushoto), hata hivyo Mhe. Majaliwa alikataa kufungua ofisi hiyo kama alivyopangiwa katika ratiba ya ziara yeke mkoani Kagera. Septemba 20, 2021, baada ya kubaini kuwa gharama za ujenzi wake ni kubwa. Kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, wa tano kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato na wa sita kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge.