Na Mwandishi Wetu
Serikali kupitia Idara ya Habari-MAELEZO imetoa siku saba (7) kuanzia leo tarehe 19 Novemba,2018 kwa wamiliki wa machapisho/majarida ambayo muda wa leseni zao umekwisha kuhuisha leseni zao.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Bw. Patrick Kipangula kwa niaba ya Mkurugenzi Idara ya Habari-MAELEZO inasema kuwa, kuendelea kuchapisha na kusambaza machapisho ambayo muda wa leseni iliyoyolewa umekwisha ni kosa kisheria na Idara haitasita kuchukua hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufuta chapisho au jarida katika orodha ya machapisho yaliyopo.
Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa, ili kupata majina ya machapisho ambayo muda wa leseni zao umekwisha tembelea tovuti ya Idara ya Habari - MAELEZO www.maelezo.go.tz sehemu ya chini kipengele cha "NIfanyeje" au kwa ufafanuzi zaidi wasiliana nao kwa namba zifuatazo 0622 664606 na 0717 312417.
Katika kutimiza utekelezaji wa matakwa ya Kifungu 5(e) cha Sheria ya Huduma za Habari na 12ya 2016 kikisomwa pamoja na kanuni zake 8(3)(4) na 12 ya Kanuni za Sheria za Huduma za Habari 2017 Tangazo la Serikali Na.18 la tarehe 3/2/2017 Idara ya Habari-MAELEZO inaendelea na zoezi la kuhuisha leseni za machapisho na majarida ambayo muda wake umefikia ukomo tangu kutolewa kwa leseni hizo.