Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kukanusha Taarifa ya Upotoshaji Inayosambaa kwenye Mitandao ya Kijamii Dhidi ya Waziri Simbachawene
Apr 01, 2020
Na Msemaji Mkuu

Kumekuwepo na taarifa ya uongo inayosambaa katika mitandao ya kijamii hapa nchini inayodai kuwa “Mhe. Mbunge wa Jimbo la Kibakwe amelazwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajali ya gari”.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inapenda kuujulisha Umma kuwa taarifa hiyo haina ukweli wowote, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George B. Simbachawene (Mb) yuko salama na anaendelea kutekeleza majukumu yake jijini Dodoma.

Aidha, Wizara inatoa onyo kali kwa mtu yeyote anayejihusisha na matukio ya uhalifu wa usambazaji   wa taarifa za uongo zenye lengo la kuzua taharuki na hofu kwa watanzania na wapiga kura wa Waziri Simbachawene.

Wizara itachukua hatua kali kwa mtu yeyote atakayebainika kuhusika na tukio hilo la kusambaza taarifa za uongo na upotoshaji wa aina yoyote.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi