[caption id="attachment_36703" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya uwekezaji Bwana Aritiside Mbwasi ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akizungumza wakati wa kongamano hilo jana.[/caption]
Na Mwandishi Wetu
Kongamano la Pili la Sekta ya Sanaa na Ubunifu ya Afrika Mashariki kuhusu Uwekezaji lenye kauli mbiu ‘Haki Ubunifu ni mali, Nikopeshe’ llilokuwa la siku mbili Oktoba 11-12, 2018 limemalizika huku wadau na Wabunifu mbalimbali kutoka Tanzania na Nchi za Afrika Mashariki wakipata kujadili changamoto katika sekta hiyo.
Awali akifungua kongamano hilo Oktoba 11,2018 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya uwekezaji Bwana Aritiside Mbwasi ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage amesema Sekta ya ubunifu ina umuhimu wake hivyo wadau wanatakiwa kuwaangalia kwa jicho la pili katika kuwasaidia wabunifu ili kuendeleza mitaji yao kwani ina umuhimu wake kwa sababu ndio inaleta biashara, huduma, bidhaa na teknolojia mpya.
Amefafanua kuwa, ni jinsi gani ubunifu unaongeza ufanisi kwa namna ya kipekee na ubunifu huo unavyofanya kazi na kuachana na kazi za mazoea.
[caption id="attachment_36705" align="aligncenter" width="750"] Bi. Hilda Twongyeirwe kutoka Uganda Women Writers Associates(FEMRITE) akiongoza mjadala juu ya haki miliki kwa wabunifu na changamoto za mitaji katika kongamano hilo.[/caption]“Wabunifu wetu wanamawazo mengi. Kwa mfano watumiaji wa Electroniki Media (digital) labda anaandaa program ya watoto namna ya kusoma ‘online’ huo ni ubunifu. Sasa changamoto taasisi za kifedha wao wanaangalia zaidi namna ada yao inavyoweza kurudi, lakini wazo au ubunifu huo aliofanya huyo msanii je Benki pengine wasiuone biashara inaweza kulipa kwa hiyo ni moja ya changamoto wanayokutana nayo wabunifu wengi nchini na kwingine kote hapa Duniani” ameeleza Aritiside Mbwasi.
Kwa hatua hiyo amebainisha kuwa, sekta hiyo inaumuhimu wake na mijadala ya kongamano hilo itakuja na hitimisho la kuwasaidia wabunifu namna ya kupata mitaji.
[caption id="attachment_36706" align="aligncenter" width="750"] Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo kutoka Uganda ambaye ni mbunifu wa mavazi, Ras Kagozi akichangia mawazo yake kwenye mijadala ya kongamano hilo.[/caption]Aidha, amesema moja ya pendekezo pengine ambalo wadau hao wanatakiwa kuangalia ni namna ya kushirikiana na wawekezaji wengine ambao tayari wao wana fedha ama mtaji ili kuingia ubia wa kuungana kwenye shea.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Maendeleo ya Afrika Mashariki la (Culture and Development East Africa - CDEA), Bi Ayeta Anne Wangusa amesema kongamano hilo lililoandaliwa kwa kushirikiano na Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) na kuwezeshwa kwa msaada wa wadau wa OSIEA na British Council, wanategemea wadau washiriki watakuja na majibu juu ya wabunifu kupata mikopo kutoka kwa wadau wenye mitaji.
Naye Mtaalmu na mtafiti wa kimaitafa wa viwanda vya ubunifu, Dkt. Keith Nurse, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirika la Dunia la Uchumi, kwenye tasisi ya Sir Arthur Lewis Institute for Social and Economic Studies ndani ya chuo kikuu cha West Indies, amesema kuwa wabunifu wengi Duniani wamekuwa na matamanio ya maendeleo makubwa lichaya kukosa fursa tarajiwa kwa wakati.
[caption id="attachment_36707" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Kiserikali la Maendeleo ya Afrika Mashariki la (Culture and Development East Africa – CDEA), Godfrey Madaraka Nyerere akibadilishana mawazo na Mwanamuziki Mkongwe nchini Mzee Kitime wakati wa kongamano hilo.[/caption] [caption id="attachment_36704" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya uwekezaji Bwana Aritiside Mbwasi akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki na wadau wa kongamano hilo la Pili la Sekta ya Sanaa na Ubunifu ya Afrika Mashariki kuhusu Uwekezaji lilokuwa la siku mbili jana Oktoba 11-12, 2018, Jijijini Dar e Salaam.[/caption]Aidha, Dkt. Nurse ametoa mifano jinisi haki ubunifu imetumika kama dhamana ya kukopesha wabunifu kutoka nchi zilizoendelea na nchi zinazoendelea.
Kongamano limeendesha mijadala mbalimbali kutoka kwa watalum wa sheria, fedha, haki miliki na haki ubunifu, kutoka Afrika Mashariki.
Aidha, wadau mbalimbali wanaoshughulikia masuala ya haki miliki kutoka serekalini na mashirika kama CISAC, wajumbe kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, Wizara zinahohusika na haki miliki toka nchi za jumuiya ya Afrika mashariki,
Benki ya Maendeleo Afrika Mashariki, Benki za kiuchuni, wawekezaji wa Afrika mashariki, mawakili wa haki miliki, vyombo vya hakimiliki vya Afrika Mashariki na wasanii mbalimbali kutoka Afrika Mashariki wameudhuria kongamano hilo.