[caption id="attachment_37911" align="aligncenter" width="755"] Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo akitoa taarifa ya mfumuko wa bei kwa mwezi Oktoba 2018 ambao umeshuka kufikia asilimia 3.2 kutoka asilimia 3.4 kwa kipindi cha mwaka unaoiushia mwezi Septemba, 2018 . hiyo ilikuwa tarehe 8 Oktoba 2018 Jijini Dodoma.[/caption]
Na: Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma
Ofisi ya Taifa ya Takwimu ‘NBS’ imetoa taarifa ya Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba ,2018 ambapo imeeleza kuwa umepungua hadi asilimia 3.2 kutoka asilimia 3.4 kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2018.
Hayo yamesema leo jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo wakati akitoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei wa mwezi Oktoba kwa ajili ya matumizi ya Serikali na wadau wa takwimu.
Kwesigabo anaeleza kuwa takwimu hiyo inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2018 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2018.
[caption id="attachment_37912" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya waandishi wa habari walikifuatilia mkutano wa kutangaza hali ya mfumuko wa Bei kwa mwezi Oktoba 2018 ambao umeshuka kufikia asilimia 3.2 kutoka asilimia 3.4 kwa kipindi cha mwaka unaoiushia mwezi Septemba, 2018 . hiyo ilikuwa tarehe 8 oktoba 2018 Jijini Dodoma. (Picha na Frank Mvungi- MAELEZO)[/caption]"Kupungua kwa Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2018 kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Oktoba, 2018 zikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba, 2017, mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Oktoba, 2018 umepungua hadi asilimia 1.2 kutoka asilimia 2.0 ilivyokuwa mwezi Septemba, 2018" amefafanua Kwesigabo
Aidha amesema kuwa, baadhi ya bidhaa ya chakula zilizochangia kupoungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na mchele kwa asilimia 3.8, mahindi asilimia 21.8, unga wa mahindi asilimia 11.6, unga wa mtama kwa asilimia 5.1, unga wa muhogo asilimia 14.1 maharage 3.0%, mihogo mibichi 5.9%, viazi vitamu 2.1, magimbi 23.2% na ndizi za kupika asilimia 11.6.
Kwa upande wa nchi za Afrika Mashariki, mfumuko wa bei kwa mwaka unaoishia mwezi octoba, 2018 nchini Kenya umepungua hadi kufika asilimia 5.53 kutoka asilimia 5.70 kwa mwaka ulioishia mwezi septemba, 2018 na mfumuko wa bei kwa mwaka unaoishia mwezi Oktoba, 2018 nchini Uganda umepungua hadi kufika asilimia 3.0 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2018.