Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kamati ya Miundombinu Yasisitiza Mazingira Mazuri Mji Mpya
Mar 13, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_51576" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mbunifu Majengo, Daud Kondoro, akiwasilisha taarifa ya utendaji wa Wakala, kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Ofisi za Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.[/caption]

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeutaka Wakala wa Majengo (TBA) kuweka hifadhi ya mazingira rafiki na ya kuvutia kwa  kupanda miti ya kivuli na matunda katika mji mpya wa Serikali wa Dodoma ili kuupendezesha mji huo.

Aidha, imeshauri wataalamu hao wawe wabunifu kwa kuwa na aina mbalimbali za michoro ya majengo kwa awamu ya pili ya mji huo kwa kufanya utafiti na kujifunza kutoka katika miji mikubwa barani Afrika na baadhi ya nchi zilizopitia hatua kama hiyo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Selemani Kakoso,  wakati Kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya ujenzi wa majengo yaliyojengwa na kusimamiwa na Wakala huo  katika mji wa Serikali wa Dodoma na kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa ofisi za Serikali - Awamu ya Kwanza na ya pili.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso, akitoa maelekezo kwa uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mara baada ya Kamati hiyo kupokea taarifa ya utendaji wa Wakala huo, kwenye ofisi za Wizara hiyo zilizopo kwenye mji wa Serikali Mtumba, Mkoani Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa. [caption id="attachment_51578" align="aligncenter" width="1008"] Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (kushoto), akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Ofisi za Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.[/caption]

Kakoso amesema kuwa  Mji wa Dodoma ni mzuri na ardhi yake inaweza kupandwa kitu chochote na kustawi kama kitasimamiwa vizuri.

"Nendeni mkajifunze kwa wenzenu waliojenga miji mipya nchi mbalimbali ili kuona tofauti ya miji ya zamani na mipya ili mnapokamilisha usanifu wa awamu ya pili kuwe na majengo yenye muonekano tofauti", amesisitiza Mwenyekiti huyo.

Kamati pia imeutaka Wakala huo kuja na mikakati madhubuti na endelevu ya ukusanyaji wa madeni ya muda mrefu na yale yanayoendelea kulimbikizwa kutokana na ada ya ushauri kutoka kwa washitiri wao kwa miradi iliyokamilika.

Kaimu Mkurugenzi wa Ushauri kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Wencelaus Kizaba akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ramani ya awamu ya pili ya usanifu wa majengo ya Serikali katika mji wa Mtumba, wakati kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa awamu ya kwanza ya Ofisi za Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. [caption id="attachment_51580" align="aligncenter" width="750"] Mafundi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakiendelea na kazi ya kuboresha miundombinu ya majengo katika mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_51581" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo na uongozi wa Wizara na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mara baada ya Kamati hiyo kupokea taarifa ya utekelezaji wa awamu ya kwanza na ya pili ya ofisi za Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.[/caption]

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Awamu ya I na II  kwa kamati hiyo, Mtendaji Mkuu wa TBA Mbunifu Majengo Daudi Kondoro amefafanua kuwa Awamu ya Kwanza imehusisha ubunifu na usanifu wa majengo madogo ya chini yenye ukubwa wa mita za mraba 1000 na yalibuniwa kuchukua viongozi wakuu wa Wizara ( Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu,  wakuu wa Idara wachache na maafisa waandamizi ).

Ameongeza kuwa mpaka sasa majengo 22 yamekamilika katika mji huo na kila moja limegharimu takribani  Shilingi Bilioni moja bila kuhusisha kazi za nje na kazi za kufunga mifumo ya TEHAMA.

Kondoro ametaja wakandarasi nane walioshiriki katika mradi huo wa awamu ya kwanza ambao ni Kikosi cha Ujenzi (TBA), Vikosi vya Ujenzi (CSWS), SUMA JKT,  Mzinga Holdings Company,  Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Kikosi cha magereza, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MUST) na Watumishi Housing Corporation (WHC).

Mtendaji Mkuu huyo wa TBA ametaja mafanikio ya mradi huo ikiwemo fursa ya wataalamu wazawa kutekeleza mradi huo kuanzia hatua ya awali ya ubunifu wa mchoro, ujenzi na usimamizi na hivyo kuwajengea uwezo watalaamu hao.

Ameongeza kuwa ujenzi wa awamu ya pili ya mji wa Serikali utahusisha usanifu na usimamizi wa majengo ya ghorofa yenye uwezo wa kuchukua watumishi wote wa Wizara na usanifu huo unatarajiwa kukamilika ifikapo  Aprili, 2020 kwa aina tatu za majengo kulingana na ukubwa wa Wizara na majukumu yanayotekelezwa.

Mnamo mwezi Septemba, 2016  Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe  Magufuli ilihamisha shughuli za Kiserikali jijini Dodoma na mwezi Juni, 2018 Wakala wa Majengo  Tanzania (TBA) ulielekezwa kufanya ubunifu na usanifu wa mji huo na walikamilisha ujenzi wa majengo hayo mwezi Aprili, 2019.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi