[caption id="attachment_51656" align="aligncenter" width="706"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akizungumza jambo na baadhi ya wananchi wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya ukaguzi wa Makama ya Hakimu Mkazi-Manyara.[/caption]
Na Karimu Meshack, Wizara ya Katiba na Sheria
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria iliyoshirikisha viongozi wa juu wa Wizara ya Katiba na Sheria na Mahakama wamefanya ziara ya ukaguzi wa majengo yanayojengwa na Mahakama ya Tanzania katika Wilaya za Kondoa mkoani Dodoma, Babati mkoani Manyara, na Longido mkoani Arusha. Aidha, ukaguzi huo pia umefanyika katika majengo ya Mahakama Kuu ya jiji la Arusha na wiki kesho utaedelea katika Mkoa wa Morogoro.
Katika ziara hiyo, Kamati imeonesha kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Mahakama ya Tanzania katika maeneo yaliyotembelewa.
Akizungumza na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini wakati wa ziara hiyo Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tabora mjini Mhe. Emmanuel Mwakasaka amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa uongozi wake mahili ambao ndiyo chachu ya ujenzi wa Mahakama nyingi nchini kwa sasa. Kondoa, Manyara, Longido ambazo zimekamilika ni mfano wa mahakama nyingi zilizojengwa na zinazoendelea kujengwa kwa kasi hapa Tanzania.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza jambo na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Emmanuel Mwakasaka wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
[caption id="attachment_51658" align="aligncenter" width="729"] Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakikagua samani katika moja ya chumba cha Mahakama ya Wilaya ya Longido jijini Arusha.[/caption] [caption id="attachment_51662" align="aligncenter" width="501"] Baadhi ya Mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la ghorofa nne la Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ambalo pia litatumika kama kituo jumuishi cha utoaji haki.[/caption] [caption id="attachment_51664" align="aligncenter" width="717"] Mheshimiwa Balozi Dkt. Augustine Mahiga akikagua samani katika jengo la Mahakama ya Wilaya ya Longido jijini Arusha.[/caption] [caption id="attachment_51666" align="aligncenter" width="617"] Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika picha ya pamoja mbele ya jengo la Mahakama ya Wilaya ya Longido, mkoani Arusha.[/caption]“Kwanza tumpongeze Mhe. Rais Dkt. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa uongozi wake madhubuti katika kuhakikisha kwamba haki inapatikana kwa haraka na kwa wakati. Kasi ya ujenzi wa majengo haya ya Mahakama ni wakupigiwa mfano, niwapongeze sana watendaji wote wa Mahakama”, amesema Mwakasaka.
Kwa upande wake, Mheshimiwa Balozi Dkt. Augustine Mahiga pamoja na kupongeza uzuri na ubora wa majengo ya Mahakama zote walizotembelea, alionesha kufurahishwa na uimara wa samani zilizowekwa katika Jengo la Mahakama ya Longido hivyo, kutoa rai kwa uongozi wa Mahakama kuzingatia utunzaji wa samani na majengo ya mahakama zote nchini hususani zilizojengwa na zinazoendelea kujengwa.
“Hizi samani zilizowekwa katika Mahakama hii ni za kiwango cha juu na zimetengenezwa kwa mbao zilizozalishwa hapa nchini na waliotengeneza ni mafundi wazawa, hongereni sana watendaji wote mliohusika kutekeleza jambo hili,” amesema Balozi Mahiga.
Ziara hii ya Kamati ya Kudumu ya Bunge katika mikoa ya Dodoma, Manyara na Arusha imeendelea leo kwa kukagua ujenzi wa Jengo la ghorofa nne la Mahakama Kuu ya Kanda ya Arusha ambalo imeelezwa pia litatumika kama kituo jumuishi cha utoaji haki. Aidha, imethibitika kwamba majengo kama hili la Mahakama Kuu ya Kanda ya Arusha yatajengwa katika mikoa ya Dodoma, Mwanza, Dar es Salaam, Morogoro na Arusha yenyewe.