[caption id="attachment_51724" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira,Mhe. Suleiman Ahmed Saddiq (Mb) (katikati) na wajumbe wengine wakimsikiliza kwa makini Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Ludovick Manege (kushoto aliyevaa koti jeusi) mara baada ya kutembelea kisima cha kuchujia maji na mafuta katika kituo cha Upimaji wa Malori yabebayo Mafuta na Dira za Maji (WMA) Misugusugu mkoani Pwani[/caption]
Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Bunge ya kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira imewapongeza kituo cha Upimaji wa Malori yabebayo Mafuta na Dira za Maji (WMA) Misugusugu mkoani Pwani kwa kutambua malengo ya Serikali kuelekea Uchumi wa Viwanda.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya ziara ya kutembelea kituo hicho Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Suleiman Ahmed Saddiq (Mb) amewataka kuendelea kujituma kwa kufata sheria na taratibu za upimaji.
“kwa kweli niwapongeze sana WMA wamefanyakazi kubwa sana na wamejiweka kisasa zaidi kwenye kila eneo hususani kuelekea Tanzania ya Viwanda, na tumejionea changamoto nyingi tukiwa kule Dodoma, leo tumekuja kupata majibu… waendele kufanya kazi” amesema Mhe. Saddiq (Mb)
[caption id="attachment_51725" align="aligncenter" width="750"] . Meneja wa Wakala wa Vipimo, Alban Kihuld akieleza jambo mbele ya Wabunge wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili kituo cha Upimaji wa Malori yabebayo Mafuta na Dira za Maji (WMA) Misugusugu mkoani Pwani ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya siku 10 kamati hiyo kutembelea viwanda.[/caption]Aidha alibainisha kuwa WMA imekuwa msaada mkubwa utatuzi wa changamoto za ubadhilifu wa mita za maji uliokuwa unafanywa na baadhi ya mamlaka husika katika lengo la kibiashara uliyosababisha kero kwa watumiaji wa mita hizo.
“nimefurahi leo nimepata majibu sahihi ya tatizo la mita za maji, mita zote lazima kabla ya kwenda kwenye mamlaka husika mfano DAWASA,DUWASA, MURUWASA lazima zote zipitie hapa WMA na kuhakikiwa kisha kupewa kibari tayari kutumika kwenye jamii” amesema Mhe. Saddiq (Mb)
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Vipimo (WMA), Ludovick Manege, amesema mafanikio ya kituo hicho yametokana na kujituma na kupata ushirikiano mkubwa kutoka Serikalini kwa kutatua baadhi ya changamoto.
[caption id="attachment_51726" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Mhe. Suleiman Ahmed Saddiq (Mb) (katikati) akielezea jambo mara baada ya kutembelea kituo cha Upimaji wa Malori yabebayo Mafuta na Dira za Maji (WMA) Misugusugu mkoani Pwani, kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Ludovick Manege[/caption]“tupo kwenye mwaka mmoja wa mafanikio ya kituo hiki kimejengwa kwa pesa za Serikali, huku ikiwa na adhama ya kuhakikisha mafuta yanasambazwa kwa vipimo sahihi na maji katika miradi mikubwa ya Serikali yanasambazwa kwa vipimo sahihi” amesema Ludovick
Aliongeza “sisi tumepewa dhamana ya kuhakikisha matenki ya mafuta yana hakikiwa hapa, yanapoenda kuchajaza mafuta, na Dira za Maji zinazoletwa nchini zote lazima zipimwe ili kuhakikisha mamlaka za maji zinatumia mita sahihi” amesema Ludovick
Kamati ya bunge ya kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira wapo kwenye ziara ya siku 10 kwa kutembelea miradi mbalimbali nchini kwa kuona changamoto na kuzichukua ili kwenda kujadiliwa bungeni.