Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

JPM Mgeni Rasmi Ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Viwanda nchi za SADC
Jul 23, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_45691" align="aligncenter" width="750"] . Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akielezea faida za maonesho ya wiki ya viwanda kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yatakayofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere kuanzia Julai 5 hadi 8, 2019 ikiwa ni sehemu ya matukio yatakaofanyika kuelekea mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa SADC.[/caption]

Na: Mwandishi Wetu - MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mageni rasmi katika ufunguzi wa maonensho ya wiki ya Viwanda  kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yatakayofanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 5, 2019

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini humo Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent   Bashungwa amewaasa Watanzania kujitokeza kwa wingi na kutumia fursa ya maonesho ya wiki hiyo yatakaofanyika kwa lengo la kuhamasisha na kukuza ujenzi wa uchumi wa viwanda na kukuza masoko kwa nchi wanachama.

“  Tayari washiriki 580 wameshajiandikisha kushiriki maonesho hayo  na matarajio yakiwa washirki zaidi ya 1000 kutoka katika nchi  wanachama wa SADC  na tunachoangalia kwa sasa ni namna maonesho ya wiki ya viwanda yatakavyowanufaisha Watanzania kwani hii ni fursa ya wazalishaji wetu na wamiliki wa viwanda kutangaza bidhaa zao na kupanua wigo wa masoko katika nchi wanachama “ Alisisitiza Mhe Bashungwa

[caption id="attachment_45692" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha ujenzi wa uchumi wa viwanda unaleta matokeo chanya hapa nchini na katika mataifa wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).(Picha zote na MAELEZO)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi