Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

JKCI Kutohusika na Mashindano ya Mbio za Heart Marathon 2020
May 28, 2020
Na Msemaji Mkuu

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuujulisha Umma kuwa haihusiki kwa njia moja au nyingine na mashindano ya mbio za Heart Marathon 2020 yaliyokuwa yafanyike  tarehe 19 Aprili mwaka huu jijini Dar es Salaam na Zanzibar na kuahirishwa kutokana na kuwepo kwa ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona (COVID – 19).

Mbio hizo za Heart Marathon ambazo zimepangwa kufanyika siku za mbeleni zimeandaliwa  na Asasi ya kiraia ya Tanzania Health Summit na siyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Aidha Taasisi inatoa rai kwa wananchi watakaopenda kushiriki katika mashindano hayo kuwasiliana moja kwa moja na waandaaji  kama matangazo yao yanavyoonesha.

Hata hivyo kama unapenda kuchangia sehemu ya gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo mdogo kiuchumi wanaotibiwa katika Taasisi yetu unakaribishwa. Unaweza kuchangia kiasi chochote cha fedha kupitia  namba ya malipo ya Serikali 994830000022.

Imetolewa na:

Anna Nkinda

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

28/05/2020

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi