[caption id="attachment_14242" align="aligncenter" width="750"] Wataalam wa Upimaji/ Wapima kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiendelea na zoezi la upimaji katika eneo la Mahina ambapo ukuta unaoonekana pichani unategemewa kuondolewa kupisha utengenezaji wa barabara za Mitaa.[/caption]
Na Mwandishi wetu – Mwanza.
Jiji la Mwanza limepima viwanja 24,000. Ikiwa ni utekelezaji wa dhana ya kuondokana na makazi holela katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza..
Akizungumzia mafanikio hayo hivi karibuni; Mratibu wa Masuala ya Urasimishaji, jijini Mwanza, Athuman Simba alisema kuwa Halmashauri ya Jiji iliunda vikosi kazi kumi na tatu (13) na kuvipangia majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na uandaaji wa michoro ya mipango miji, upimaji, ukaguzi wa viwanja na kumilikisha.
Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza; Hosiana Kusiga amesema kuwa kati ya viwanja 24,000.vilivyopimwa viwanja 19,417 vipo kata za Buhongwa, Mkolani, Igoma, Mhandu, Luchelele, Mahina, Isamilo, na Nyegezi..
[caption id="attachment_14245" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Mtaa wa Ipuli, Kata ya Mahina; Rajabu Jumanne (mwenye shati la bluu) akishuhudia zoezi la upimaji linavyoendelea katika Mtaa wake, likiongozwa na Mratibu wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza,.Yohana Cleophace.[/caption] [caption id="attachment_14248" align="aligncenter" width="750"] : Muonekano wa Barabara iliyochongwa rasmi na Wataalam wa Upimaji/ Wapima kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiendelea na zoezi la Urasimishaji katika kata ya Ipuli, Mahina.[/caption]Aidha, viwanja 5,515 vimefanyiwa upimaji wa awali na kazi hiyo inaendelea katika kata za Butimba, Mahina, Mkolani, Lwahnima, Igoma, Mhandu, Kishiri na Luchelele. ambapo jumla ya viwanja vilivyokamilika na vilivyo kwenye upimaji wa awali ni 25,032..
Utekelezaji wa upimaji huo unatokana na agizo la Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Mhe. William Lukuvi, kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, ambapo alilitaka kuandaa hati miliki za viwanja 35,000 kupitia mradi wa urasimishaji makazi holela.