Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Jaji Mkuu Akitaka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Kufanya Tafiti
Dec 10, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_38749" align="aligncenter" width="800"] Jaji Mkuu wa Tanzania Prof.Ibrahim Hamis akizungumza wakati akizindua Baraza la tatu la wafanyakazi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Leo Jijini Dodoma.[/caption]

Jaji mkuu wa Tanzania Mh. Ibraham H. Juma, amekitaka Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kufanya tafiti na kutoa ushauri wa namna ya kuondoa migongano ya kisheria wakati Mahakama ikiendelea kuangalia namna bora ya kusimamia sheria ili kupunguza au kuondoa kabisa migongano hiyo.

Mh. Jaji Mkuu ametoa agizo hilo leo wakati akizindua baraza la tatu la wafanyakazi la Chuo Cha (IJA), katika hafla ya uzinduzi wa balaza hilo, iliyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Kumbukumbu Tuli cha Taifa jijini Dododma.

Kupitia hotuba yake Mh. Jaji Mkuu, mbali na kuzitambua changamoto zinazokikabili Chuo hicho, ikiwemo upungufu wa vitendea kazi na watumishi kwa kada ya utawala, aliwakumbusha watumishi wa Chuo hicho kuzingatia uadilifu katika kutekeleza shughuli zao za kila siku.

[caption id="attachment_38747" align="aligncenter" width="800"] Jaji Mkuu wa Tanzania Prof.Ibrahim Hamis akizungumza wakati akizindua Baraza la tatu la wafanyakazi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Leo Jijini Dodoma.[/caption]

“Tunawajibika kufanya kazi kwa weledi, uthubutu na uadilifu wa hali ya juu, ili tuwawakilishe vyema wale waliotuamini sambamba na kuiwezesha serikali kufikia malengo yake ya kukuza uchumi wa viwanda na kuondoa umasikini” alisistiza Mh. Jaji Mkuu.

Mh. Jaji Mkuu aliwaasa kujiepusha na vitendo vya rushwa, utoro mahali pa kazi, na uzembe wa namna yoyote ile, kwani kushiriki vitendo vya namna hiyo ni kukitia doa Chuo, Mahakama, Utunishi wa Umma na Taifa kwa ujumla.

[caption id="attachment_38751" align="aligncenter" width="800"] Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis akimsikiliza Mwenyekiti wa Raawu Bw.George Banoba kutoka chuo Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto mara baada ya Jaji Mkuu mkuu uyo kuzindua Baraza la tatu la wafanyakazi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Leo Jijini Dodoma.[/caption]

“Mkumbuke pia, mabadiliko yanayofanywa na Mahakama ya Tanzania katika Utendaji na ambayo yanakigusa Chuo chetu cha Mahakama ni pamoja na kujenga nidhamu, weledi na uwajibikaji mahali pa kazi, hivyo hakikisheni mpango mahususi unawekwa katika kutimiza adhima hiyo” Alisema jaji Mkuu.

 Chuo cha Uongozi wa Mahaka Lushoto (IJA) kinatambulika kimataifa katika kubuni, kuandaa na kuendesha mafunzo ya kimahakama, kwa ajili ya Majaji, Mahakimu, Wanasheria wa Serikali,  Waendesha Mashitaka, Maafisa wa Jeshi la polisi na Magereza, Watendaji wa Serikali za Mitaa, pamoja na makundi yote yanayojihusisha utoaji haki.

IJA kama lilivyo jina lake ni Chuo kilichopo chini ya Mahakama ya Tanzania, na kinafanya kazi kwa usimamizi wa Mahakama na Wizara ya Katiba na Sheria. Pia, kinafanya tafiti mbalimbali za kisheria, na kutoa ushauri katika masuala mbalimbali yanayohusu utoa haki kwa umma. Aidha, kinafanya shughuli zake kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za mafunzo za ndani na nje ya nchi.

[caption id="attachment_38750" align="aligncenter" width="800"] Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto wakifuatilia hotuba ya Jaji Mkuu wa Tanzania Prof.Ibrahim Hamis(hayupo pichani) wakati akizindua Baraza la tatu la wafanyakazi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Leo Jijini Dodoma.[/caption]  

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi