[caption id="attachment_10270" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akielezea jambo alipotembelea mradi wa ujenzi wa Kituo cha mafunzo kwa ajili ya wadau wa Mahakama leo Jijini Dar es Saalaam. Kituo hicho kinajengwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kitakuwa kikitumiwa na Taasisi ya Uongozi wa Mahakama (IJA) katika kutoa mafunzo kwa njia ya teknolojia ya kiasa. Kushoto kwake ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania (WB) Bi. Bella Bird na Mtaalamu wa Benki ya Dunia (WB) Bw. Waleed Malik (kulia).[/caption]
Na: Frank Shija
Mahakama imeanzisha Kituo cha mafunzo kwa lengo la kusogeza huduma za mafunzo kwa wadau mbalimbali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa maboresho ya Mahakama nchini.
Hayo yamebainishwa leo na Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma alipotembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha mafunzo kinachojengwa katika Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.
[caption id="attachment_10273" align="aligncenter" width="750"]Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo Kaimu Jaji Mkuu Mhe. Profesa Ibrahim Juma amesema kuwa kituo hicho kitasaidi sana kwa mahakimu, majaji, waendesha mashtaka, wapelelezi na wadau wengine kupata mafunzo wakiwa katika maeneo yao kwa ukaribu zaidi badala ya kusafiri hadi Chuo cha Uongozi wa Mahakama kilichopo Lushoto Tanga.
“ Tunaanzisha Kituo hiki hapa Dar es Salaam kitakachotumika kutoka mafunzo kwa Mahakimu, Wapelelezi, Majaji, wadau wetu wakiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hata nyie Waandishi wa Habari mtapata fursa hiyo,” alisema Mhe. Profesa Ibrahim.
Kwa upande wake Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia (WB) Waleed Malik amesema kuwa amefurahishwa na namna ujenzi huo unavyoendelea na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mahakama katika kutekeleza mpango mkakati wa miaka mitano wa Mahakama unaoenda sambamba na maboresho ya huduma za Mahakama.
[caption id="attachment_10274" align="aligncenter" width="750"]Naye Mratibu wa mpango huo Mhe. Zahara Maruma amesema kuwa kituo hicho kitakuwa kikitumia teknolojia ya kisasa katika utoaji wa mafunzo kupitia njia ya video conference ambapo wawezeshaji watatumia kituo hicho kuwasiliana moja kwa moja na wanafunzi wakiwa katika maeneo yao.
Mhe. Zahara amesema kuwa lengo kubwa la Mahakama ni kuunganisha Mahakama zote katika mfumo wa video conference ambazo zitawezesha watumishi kupata mafunzo wakiwa katika maeneo yao ya kazi.
Aliongeza kuwa kukamilika kwa kituo hicho kusaidia katika kutunza muda, na gharama zilizokuwa zinatumiwa kwa ajili ya mafunzo kwa kuwa watumiaji wa mahakama watapata huduma hiyo wakiwa katika maeneo yao ambapo Mahakama zao zitakuwa na mtandao wa video.
[caption id="attachment_10279" align="aligncenter" width="750"]“ Mfumo huu utaondoa ulazima kwa majaji na wadau kwenda Lushoto kwa ajili ya mafunzo badala yake watapata mafunzo kupitia mtandao wa Video Conference wakiwa maeneo yao moja kwa moja kutoa hapa au Lushoto” alisema Mhe. Zahara.
“Kukamilika kwa Kituo hiki kutatoa fursa kwa uanzishwaji wa vituo vingine kama hiki katika maeneo mengine ya hasa katika Mahakama Kuu za Kanda,” aliongeza.
Ujenzi wa kituo hiki unagharimu jumla ya shilingi milioni 78 chini ya ufadhiri wa Benki ya Dunia ambapo ujenzi wake utachukua muda wa wiki nane kutokana na kutumia teknolojia ya kisasa ya ujenzi nafuu ijulikanyo kama Moladi. Kituo hiki kitakuwa kikitumiwa na Taasisi ya Uongozi wa Mahakama (IJA) kilichopo Lushoto katika kutoa mafunzo kwa wadau wa Mahakama.