Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Hifadhi ya Ngongoro Kuendelea Kuvutia Watalii Zaidi- Dkt Manongi
Apr 20, 2019
Na Msemaji Mkuu

 

Na Frank Mvungi

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kuendelea kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi ili kuongeza mchango wa sekta hiyo katika pato la Taifa na kuchochea ustawi wa wananchi.

Hayo yamesemwa na Mhifadhi mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Fredy Manongi wakati wa kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’  ambapo alieleza kuwa dhamira ya Mamlaka hiyo ni kuendelea kubuni mbinu mpya za kutangaza vivutio vilivyomo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ambavyo havipaatikani katika maeneo mengine Duniani wakiwemo wanyama, makundi ya ndege na kreta.

“ Serikali ilichukua hatua za makusudi wakati inaanzisha Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ili kulinda urithi huu wa Taifa na Dunia kwa ujumla ili uweze kunufaisha kizazi cha sasa na vizazi vijavyo” Alisisitiza Dkt. Manongi

Akifafanua amesema kuwa kutokana vivutio vilivyopo katika Hifadhi hiyo kuwa vya kipekee hali hiyo imepelekea kuongezeka kwa watalii wanaotembelea eneo hilo kila mwaka kutoka ndani nan je ya nchi hali inayochangia kuongeza mapato yanayotokana na utalii.

Pia Dkt Manongi alitoa wito kwa watanzania kutumia fursa ya vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchini kwa kutembelea vivutio hivyo ikiwemo ngorongoro ili kuchangia katika kukuza utalii wa ndani na kuwezesha sekta hiyo kutoa mchango stahiki katika kukuza uchumi.

Aidha, Dkt Manongi alibainisha kuwa Mamlaka hiyo imetenga Bilioni 9 kwa ajili ya ujenzi wa barabara kutoka kuwa za vumbi hadi kiwango cha  simenti ili kuimarisha miundombinu  ndani ya hifadhi hiyo.

Hifadhi ya Ngorongoro imeanzishwa mwaka 1959 ikiwa ni moja ya maeneo yanayotambulika kama urithi wa dunia na imekuwa kivutio kikubwa kwa wageni kutoka ndani nan je ya nchi kutokana na vivutio vilivyomo wakiwemo wanyama wa aina mbalimbali na ndege wa pekee ambao hawapatikani katika maeneo mengine.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi