Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Hayati Karume Kielelezo cha Uwazi na Uadilifu
Apr 04, 2019
Na Msemaji Mkuu

Na; Mwandishi Wetu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Hayati Mzee Karume ni kielelezo cha misingi ya falsafa za uwazi, uadilifu, ushirikishwaji, upendo, amani na ubunifu ambazo ni tunu alizoishi nazo kipindi cha maisha yake ya ujenzi wa taifa la Zanzibar.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo leo wakati wa akifungua wa kongamano la pili la maadhimisho ya kumbukumbu ya Rais na Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar hayati Abeid Amani Karume linalofanyika kwenye Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, kampasi ya Zanzibar Bububu. 

[caption id="attachment_41784" align="aligncenter" width="900"] : Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Pili la Maadhimisho ya kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume linalofanyika kwenye Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Zanzibar Bubu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)[/caption]

Hayati mzee Karume alifanikiwa kuweka misingi ya utendaji wenye kuacha alama katika maisha na mifumo mbalimbali ya kiserikali ambapo katika kipindi chake cha uongozi alifanya mambo mengi ambayo hadi leo hii yamebaki kuwa kielelezo cha uongozi wake.

“Tutumie muda huu kutafakari hekima, busara na falsafa za mzee Karume kwa maendeleo na mustakabali wa Zanzibar na wananchi wake”alisema Makamu wa Rais

Aidha, Makamu wa Rais amewataka viongozi wa sasa kujifunza kutoka kwa viongozi waasisi wa taifa ambao walijitolea na kutumikia wananchi kwa kuzingatia misngi wa haki na usawa.

“Mwaka huu tunaadhimisha miaka 47 tangia mzee wetu atangulie mbele za haki viongozi wa Zanzibar hatuna budi kujitafakari na kujitathmini kwa kina kama tunayofanya ni ndio au siyoalisisitiza Makamu wa Rais Suluhu.

Makamu wa Rais amemuelezea mzee Abeid Karume kuwa ni kiongozi aliyethamini uwajibikaji na kuzingatia ilani ya chama cha Afro Shiraz iliyohakikisha Zanzibar inapata maendeleo na alichukizwa sana na vitendo vya rushwa, ubadhirifu, uzushi na uongo.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho, ndugu Stephen Wasira, amesema chuo hicho ni chuo pekee kinachofanya kazi ya kuyaenzi mazuri yaliofanywa na waasisi wa nchi ya Tanzania na kuwafundisha vongozi na vijana umuhimu wa kuyaenzi mazuri yote yaliyofanywa na waasisi wan nchi yao.

Naye mjane wa mzee karume mama Fatuma Karume alitumia nafasi ya kusalimia waliohudhuria kongamano hilo kwa kuwataka wanawake kuendelea kushikamana na waweze kushiriki vyema kwenye harakati za kuiletea nchi maendeleo. Alitoa mfano namna alivyopigania haki ya wanawake kupiga kura na leo anayo furaha kushuhudia mwanamke kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi