Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Hasunga Aagiza Wasambazaji wa Viuatilifu Feki Kunyang’anywa Leseni
Mar 28, 2019
Na Msemaji Mkuu

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wakati akifungua kongamano la siku tatu la Kitaifa la Kisayansi kuhusu Bioanuwai, Visumbufu na matumizi sahihi na salama ya teknolojia za viuatilifu linalofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kusimamia na kudhibiti Viuatilifu-TPRI Jijini Arusha, leo tarehe 28 Machi 2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo – Arusha

Sanjari na matumizi sahihi na salama ya viuatilifu na uhifadhi wa mazingira yanayotuzunguka, bado sekta ya viuatilifu imekuwa na changamoto nyingi.

Kutokana na ukubwa wa nchi ya Tanzania na mipaka yake sambamba na kupakana na nchi nyingine nyingi  pamekuwapo na upitishwaji usio rasmi wa viuatilifu katika mipaka na hususani kwa mikoa ya mipakani unaofanywa na wafanyabiashara na wananchi wasiowaaminifu. Hali hiyo imepelekea  kuwepo kwa viuatilifu visivyo na ubora kwa wakulima kwa baadhi ya maeneo.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 28 Machi 2019 wakati akifungua kongamano la siku tatu la Kitaifa la Kisayansi kuhusu Bioanuwai, Visumbufu na matumizi sahihi na salama ya teknolojia za viuatilifu linalofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kusimamia na kudhibiti Viuatilifu-TPRI Jijini Arusha.

Baadhi ya washiriki wa kongamano la siku tatu la Kitaifa la Kisayansi kuhusu Bioanuwai, Visumbufu na matumizi sahihi na salama ya teknolojia za viuatilifu linalofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kusimamia na kudhibiti Viuatilifu-TPRI Jijini Arusha wakifatilia hotuba ya Mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, leo tarehe 28 Machi 2019.
 
Mhe Hasunga amewataka Wakaguzi wa viuatilifu wa TPRI, Maafisa ugani pamoja na vyombo vya dola  kushirikiana kwa karibu katika kubaini ufumbuzi wa jambo hilo na punde watakapowabaini waagizaji na wasambazaji wa viuatilifu feki nchini kuwanyang’anya leseni zao sambamba na kuwachukulia hatua za kisheria.
 
Kadhalika, TPRI imetakiwa kutojihusisha na rushwa katika usajili wa viuatilifu nchini na endapo kuna mtendaji atabainika akijihusisha na rushwa ya uzembe ama kitaaluma atachukuliwa hatua kali za kisheria.
 
Pia amewataka TPRI kuhakikisha kuwa wanasimamia uteketezaji wa viuatilifu vyote ambavyo vimebainika kuwa feki sambamba na kuandaa mpango maalumu wa utekelezaji wa majukumu hayo.
 
Alisema kupitia mpango wa TPRI  wa kufungua Ofisi na matawi yake katika Kanda nne nchini zikiwepo Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kusini na Kanda ya Kaskazini, kutekleza vyema majukumu yake ili kubaini na kuwachukulia hatua kali za kisheria wahujumu wa uingizaji na usambazaji wa viuatilifu kwa wakulima nchini.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizindua tovuti wakati akifungua kongamano la siku tatu la Kitaifa la Kisayansi kuhusu Bioanuwai, Visumbufu na matumizi sahihi na salama ya teknolojia za viuatilifu linalofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kusimamia na kudhibiti Viuatilifu-TPRI Jijini Arusha, leo tarehe 28 Machi 2019.
Alisema mkakati huo utaowaongezea uwezo katika  kupambana na tatizo hilo la uingizaji wa viuatilifu kwa njia za panya.
 
“Kuna madhara makubwa kwa mwananchi mmojammoja na Taifa kwa ujumla wake kutokana na usambazaji wa viuatilifu feki hivyo kama Waziri mwenye dhamana ya kusimamia sekta ya kilimo nitahakikisha tunaikabili na kubaini chanzo chake ili kuiondoa changamoto hii” Alikaririwa Mhe Hasunga
 
Alisema, Sekta ya Kilimo imendelea kuwa ni mhimili  mkubwa wa uchumi wa Tanzania na katika mwaka 2017 sekta hiyo imetoa ajira kwa asilimia  65.5 na kuchangia asilimia 65 ya malighafi za viwanda. Aidha , mchango wa sekta katika pato la Taifa ni asilimia 30.1 ambapo Sekta ndogo ya mazao imechangia asilimia 17 pekee.
 
Kutokana na umuhimu huo, Serikali inaendelea kutekeleza mikakati ya kuongeza kasi ya kukuza kilimo, ili kuchochea na kufikia uchumi wa viwanda sawa sawa na Azma ya Serikaliya Awamu ya Tano. 
 
Mhe Hasunga alisema kuwa Mabadiliko ya tabia nchi ni mtiririko wa mfumo wa mabadiliko ya hali ya hewa yanayochukua muda mrefu au mfupi na kusababisha hali mbaya za hewa ama uchache wa hali inayohitajika au wingi wa hali isiyohitajika na kusababisha madhara kwa jamii na nchi kwa ujumla.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wakati akifungua kongamano la siku tatu la Kitaifa la Kisayansi kuhusu Bioanuwai, Visumbufu na matumizi sahihi na salama ya teknolojia za viuatilifu linalofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kusimamia na kudhibiti Viuatilifu-TPRI Jijini Arusha, leo tarehe 28 Machi 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua mbegu mbalimbali mara baada ya kutembelea kampuni ya wazalishaji na wasambazaji wa mbegu bora  ya Suba Agro wakati wa kongamano la siku tatu la Kitaifa la Kisayansi kuhusu Bioanuwai, Visumbufu na matumizi sahihi na salama ya teknolojia za viuatilifu linalofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kusimamia na kudhibiti Viuatilifu-TPRI Jijini Arusha, leo tarehe 28 Machi 2019.
Kwa zaidi ya miaka 50, hali ya hewa duniani imekuwa ikibadilika kwa sababu ya kuongezeka gesi chafu zinazozalishwa na mvuke wa maji, methane na  kaboni  dayoksaidi, hasa kutokana na kuungua kwa mafuta na  makaa ya mawe, ukataji  hovyo wa miti na shughuli nyingine za kibinadamu kama kilimo, Ukuaji wa miji na uchimbaji wa madini.
Hali hii ya mabadiliko ya tabia nchi imesababisha kuwepo kwa ongezeko la visumbufu vya mazao kama vile wadudu kuzaliana kwa wingi kutokana na ongezeko la joto, kuingia kwa magonjwa mapya ya mazao kama (Maize necrosis), Viwavi jeshi vamizi (Fall army worms) kuenea kwa magugu vamizi na hata ongezeko la mbu kwa mikoa na miji ile iliyokuwa na hali ya baridi miaka ya nyuma.
 
Kongamano hilo la siku tatu litakuwa na muktadha wa kujadili Bioanuwai, Visumbufu na Matumizi Sahihi na Salama ya Teknolojia za Viuatilifu katika kukuza kilimo ili kujenga Tanzania ya Viwanda. Na kuwa na mawasilisho katika nyanja za Ubunifu na Ugunduzi wa Teknolojia na mbinu mbalimbali  katika kudhibiti visumbufu vya mazao yakiwa shambani na ghalani; Teknolojia katika uzalishaji viuatilifu na madhara ya mabaki yake katika mzingira; Matumizi ya Viuatilifu katika kudhibiti wadudu waenezao magonjwa ya binadamu na mifugo; Masuala ya kisheria katika matumizi  sahihi na salama ya viuatilifu na Matumizi endelevu ya bioanuwai katika kukuza viwanda.
   

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi