Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt: Shein: Jitihada za Kuimarisha Mazingira ya Mahakama Ziende Sambamba na Ufanisi Katika Utoaji wa Huduma
Sep 27, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_15794" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Katiba, Sheria na Utawala Bora toka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Haruna Ali Suleiman akizungumza kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dkt. Mohamed Ali Shein katika hafla ya kufunga mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu toka nchi wananchama wa Jumiya ya Madola (CMJA) leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na: Frank Shija)[/caption]

Na. Paschal Dotto

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema jitihada zinazochukuliwa na serikali za nchi za Jumuiya ya Madola kuimarisha mazingira ya kazi katika Mahakama hazina budi kwenda sambamba na kuimarika kwa utendaji wa mahakama hizo katika kutoa huduma kwa wananchi.

Katika hotuba yake kufunga mkutano wa siku tatu wa Chama cha Majaji na Mahakimu cha nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola leo, Dk. Shein amesema ni kweli kuwa Serikali ina wajibu mkubwa katika kuimarisha mazingira ya kazi katika mahakama lakini pia mahakama zinapaswa kutimiza wajibu wake ipasavyo.

[caption id="attachment_15795" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) Jaji John Lounders akizungumza kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dkt. Mohamed Ali Shein katika hafla ya kufunga mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu toka nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Jaji Omary Othmani Makungu, Waziri wa Katiba, Sheria na Utawala Bora toka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Haruna Ali Suleiman na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma.[/caption]

“Majaji na Mahakimu ni watu muhimu katika jamii kwani mmepewa nguvu kubwa na wajibu wa kipekee katika kufanya maamuzi yanayogusa mustkabala wa pande zinazohusika katika mashauri mnayoyaamua hivyo ni lazima wakati wote mufuate sheria na kutekeleza majukumu yenu kwa uhuru na kwa kuzingatia maadili ya kazi yenu” alisema Dk. Shein.

Katika hotuba yake hiyo iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Sheria, Katiba na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Haroun Ali Suleiman, Dk. Shein alieleza kuwa chama hicho cha Majaji na Mahakimu wa nchi za Jumuiya ya Madola ni moja ya taasisi zinazopigia chapuo uhuru na hadhi ya mahakama, utoaji haki na utawala wa sheria tangu kuasisiwa kwake mwaka 1972.

[caption id="attachment_15796" align="aligncenter" width="750"] Kutoka kushoto ni Waziri wa Katiba, Sheria na Utawala Bora toka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Haruna Ali Suleiman, Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma na Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) Jaji John Lounders wakiimba wimbo wa Taifa la Tanzania wakati hafla ya kufunga mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu toka nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Dk. Shein alitoa wito wa ushirikiano baina ya mahakama za nchi za Jumuiya ya Madola katika kukabiliana na changamoto mbali mbali ikiwemo vitendo vya kigaidi, usafirishaji haramu wa binadamu, usafirishaji fedha haramu, uharamia na uvuvi haramu pamoja na vitendo vingine hatarishi kwa maendeleo na uhai wa binadamu na kusisitiza kuwa “Tunahitaji mahakama zenye nguvu ili kuweza kushinda vita hivi”

Aliongeza kuwa Mkutano huo ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi wanachama kwa kuwa umetoa fursa kubwa ya kujadili changamoto zinazozikabili nchi hizo hususan katika “mifumo yetu ya mahakama kama kucheleweshwa kwa kesi, maadili ya mahakama na kuimarisha mazingira ya kufanyia kazi kwa maofisa wetu kwa hiyo kubadilishana mawazo katika sehemu hizi kutaimarisha zaidi utendaji kazi”

[caption id="attachment_15797" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya washiriki wa mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu toka nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar Dkt. Mohamed Ali Shein iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Katiba, Sheria na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Haruna Ali Suleiman leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na: Frank Shija)[/caption]

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ignas Kitusi alieleza matumaini yake kuwa kutokana na mada zilizowasilishwa katika mkutano huo, maadili ndani na nje ya mahakama yataimarika na kuleta utendaji kazi mzuri kwa mahakama ya Tanzania.

Alibainisha kuwa katika mkutano ujao ambao unatarajiwa kufanyika nchini Australia, washiriki watapata fursa ya kujithmini namna walivyotekelza maazimio yaliyopitisha katika mkutano wa Dar es salaam.

Miongoni mwa maazimio yaliyopitishwa ni pamoja na kuyafanyia kazi maeneo mapya ya sheria ya ugaidi, ujangili pamoja na sheria ya mtandao.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi