[caption id="attachment_46259" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza wakati alipofunga mashindano ya Michezo kwa shule za msingi na sekondari za Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika kuanzia Agosti 16 -24 Agosti Jijini Arusha.[/caption]
Na Shamimu Nyaki –WHUSM.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe amefunga mashindano ya kumi na nane ya michezo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa shule za msingi na sekondari (FEASSA) yaliyofanyika Jijini Arusha.
Akizungumza katika kuhitimisha Mashindano hayo Mhe. Mwakyembe ameeleza kuwa Tanzania mwaka huu imekuwa na bahati kubwa katika kufanya matukio ya kimataifa ambapo amewapongeza watanzania kwa kuonyesha uzalendo wa hali ya juu na kutunza amani na utulivu kipindi hicho na kuwaomba kuendelea kufanya hivyo.
[caption id="attachment_46260" align="aligncenter" width="930"] Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Bibi. Odilia Mushi akizungumzia mafanikio ya mashindano ya Michezo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa shule za msingi na sekondari kuanzia Agosti 16 -24 Agosti Jijini Arusha.[/caption] [caption id="attachment_46261" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Michezo kwa shule za msingi na sekondari kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw.George Omond akizungumza wakati wa ufungaji wa mashindano ya Jumuiya hiyo yaliyofanyika kuanzia Agosti 16 -24 Agosti Jijini Arusha.[/caption]“Mwaka huu nchi yetu imepokea wageni wengi katika matukio ya kimataifa ambayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa nawapongeza watanzania kwa kufanikisha hili na niendelee kuwasisitiza kulinda amani na kuonyesha ukarimu wa hali ya juu kwa wageni wote wanaingia nchini”alisema Mhe.Mwakyembe.
Aidha ameongeza kuwa michezo kwa wanafunzi ina nafasi kubwa ya kuibua vipaji walivyonavyo ambavyo vitawasaidia katika maisha yao kwakua Michezo imekua ni ajira rasmi katika dunia ya leo.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya ya Rais TAMISEMI Bibi.Odilia Mushi amesema kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na FEASSA wamefanya kazi kubwa katika kuhakikisha mashindano hayo yanafanikiwa na kuendelea kusisitiza ushirikiano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki uendelee kuimarika kwa maslah ya nchi wanachama.
[caption id="attachment_46262" align="aligncenter" width="936"] Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Bibi. Odilia Mushi akigawa zawadi kwa washindi wa mpira wa miguu kwa wasichana kutoka Tanzania katika mashindano ya Michezo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa shule za msingi na sekondari kuanzia Agosti 16 -24 Agosti Jijini Arusha.[/caption] [caption id="attachment_46263" align="aligncenter" width="750"] Timu ya mpira wa miguu kwa wasichana kutoka Tanzania wakishangilia ushindi wa mchezo katika mashindano ya Michezo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa shule za msingi na sekondari kuanzia Agosti 16 -24 Agosti Jijini Arusha.[/caption]Naye Naibu Katibu Mkuu wa FEASSA Bw.Geoge Omond amesema kuwa kuanzia mwaka ujao mashindano hayo yatahusisha shule za sekondari pekee ambapo jina la mashindano hayo litabadilika na kuwa Shirikisho la Michezo kwa shule za Sekondari za Jumuiya ya Afrika Mashariki yaani (FESSA) na mwenyeji wa mashindano hayo atakuwa nchi ya Kenya.
Bw.Omond amesema kuwa lengo la kubadilisha mashindano hayo ni kutoa nafasi zaidi kwa shule za sekondari ambazo wanafunzi wake tayari wanakuwa na umri ambao utawasaidia katika kutumia michezo kama ajira.
Mashindano hayo yamehusisha shule mbalimbali za msingi na sekondari za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo yamefanyika kwa siku kumi Jijini Arusha ambapo washindi wa jumla ni Nchi ya Uganda na Tanzania imeshika nafasi ya tatu.