[caption id="attachment_51832" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipima joto la mwili kabla ya kuingia katika ukumbi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kwa ajili ya kupokea Taarifa ya CAG kwa Mwaka 2018/2019 pamoja na Taarifa ya TAKUKURU leo tarehe 26/03/2020.[/caption]
Na Jonas Kamaleki, Dodoma
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) imeokoa jumla ya Shilingi bilioni 1.45 ambayo ingelipwa kama ada ya ukaguzi kwa makampuni binafsi ya ukaguzi.
Hayo yamebainishwa leo Ikulu ya Chamwino, Dodoma na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Charles Kichere wakati akiwasilisha Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2018/19 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
[caption id="attachment_51833" align="aligncenter" width="750"]Kichere amesema ofisi yake imeokoa fedha hizo kwa kutumia wakaguzi wa ofisi yake kukagua mashirika ya umma ambayo baadhi yake ni TANAPA, BOT, SUA, TTCL na TIC.
“ Mheshimiwa Rais ofsi yangu imejipanga kukagua mashirika mengine makubwa kama vile Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro, EWURA, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Tanesco, Chuo Kikuu cha Ardhi, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),” amesema Kichere.
[caption id="attachment_51834" align="aligncenter" width="750"]Kutokana na uhaba wa watumishi katika ofisi ya CAG, Rais Magufuli ameiagiza Utumishi kutoa kibali cha ajira ya watumishi 25 katika ofisi hiyo.
“CAG nakupongeza sana kwa kuanza kukagua mashirika yetu ya umma kwa kutumia watu wetu, ni kitendo cha kizalendo, umefanya vizuri,” amesema Rais Magufuli
Aidha, Rais Magufuli amemthibitisha aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kumpambana na Rushwa (TAKUKURU), Brigedia Jenerali, John Mbungo kuwa Mkurugenzi MKuu wa TAKUKURU kutokana na kazi aliyoifanya ya kurudisha bilioni 8.8 za wananchi.
[caption id="attachment_51836" align="aligncenter" width="750"]Rais Magufuli amemuhakikishia Mhe. Spika, Job Ndugai kuwa Ripoti ya CAG itawasilishwa bungeni jinsi ilivyo bila kubadilishwa kwa namna yoyote ili ijadiliwe na wabunge kwa mujibu wa sheria.
CAG na TAKUKURU wamewasilisha Ripoti zao leo kwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu ya Chamwino Dodoma.
[caption id="attachment_51837" align="aligncenter" width="750"]