[caption id="attachment_42311" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wakati wakichangia Hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambayo imeidhinishwa leo leo Aprili 23,2019 na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma.[/caption]
Na Shamimu Nyaki – WHUSM
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeidhinisha Bajeti ya Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo yenye kiasi cha Shilingi Bilioni thelathini,Milioni Mia Nane Sabini na Tisa,Mia Nne Themanini na Tatu Elfu (30,879,483,000) kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya Wizara.Akijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wakati wakuchangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alisema kuwa Wizara yake itaendelea kutekeleza Miradi ya Maendeleo pamoja na majukumu yote yaliyopo katika Sekta zake.
“Serikali itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa ikiwemo kusimamia Maadili na Utamaduni wa Taifa Letu,kusimamia Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 pamoja na kusimamia michezo hapa nchini,” alisema Dkt.Mwakyembe.
Pamoja na hayo Mheshimiwa Dkt.Mwakyembe ameliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kutengeneza Kanuni zitakazosaidia uendeshaji wa Uwakala wa Wanamichezo hapa nchini ili kusaidia Wanamichezo kuendeleza vipaji vyao na kujitangaza kimataifa.
[caption id="attachment_42314" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wakati wakichangia Hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambayo imeidhinishwa leo leo Aprili 23,2019 na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe.[/caption]Halikadhalika nae Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amesema kuwa Serikali inaendelea na mazungumzo na Kampuni ya Beijing Constructions Engineering kuhusu kuhuisha mkataba wa Usimamizi wa Uwanja wa Taifa.
[caption id="attachment_42316" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara hiyo baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 leo Aprili 23,2019 Jijini Dodoma.[/caption]Vilevile Mhe.Naibu Waziri huyo amesema kuwa Serikali inaendelea kuimarisha usikivu wa TBC pamoja na Kuboresha Shirika la Magazeti ya Serikali ambalo kwa sasa lina Chaneli ya Mtandao Daily News Digital,aidha ameeleza namna Serikali inavyojipanga kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi ambapo tayari kiasi cha Shilingi Bilioni 3.2 zimetumika kulipa madeni ya watumishi wa Shirika hilo. Naye Mhe.Juma Nkamia (Mb.) ameishauri Serikali kutoa fedha zilizopitishwa kwa ajili ya Wizara hiyo ili iweze kutekeleza majukumu yake vizuri kwa kuwa ni Wizara inayogusa wananchi moja kwa moja.