Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

BOT Kuanzisha Mfumo wa Malipo ya Papo kwa Papo
Dec 14, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO Dodoma

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) inatarajia kuanzisha mfumo mpya wa malipo ya papo kwa papo (TIPS) mapema januari 2019 kwa lengo la kurahisisha huduma hiyo kwa wadau wake.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Lucy Shaidia wakati akaiwakilisha mada ya mfumo wa malipo ya papo kwa papo, kwa waandishi wa habari za uchumi na fedha jijini Dodoma.

"Utaratibu mfumo mpya wa malipo ya papo kwa papo utapunguza matumizi ya fedha taslimu na hivyo kutoa njia mbadala ya kufanya malipo na mfumo huu kwawakati, haraka na salama.

Aidha aliongeza kuwa, BoT inategemea utekelezaji wa mfumo huo mpya wa malipo ya papo kwa papo  kufanyika nchi nzima ambapo ifikapo Juni 2020 mfumo huo wa malipo ya papo kwa hapo utakuwa umekamilika nchi nzima.

Hata hivyo Bi Shaidi alieleza sababu za kuanzishwa kwa mfumo huo, na kusema kuwa BoT kama msimamizi wa taasisi za fedha, imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inaleta ufanisi katika matumizi ya miundombinu iliyopo ya malipo ya fedha kupitia mitandao ya simu ikiwa ni pamoja na kuyataka makampuni ya simu kuwa na mfumo utakaowezesha wateja wao kutoka mitandao tofauti kuweza kufanya malipo bila usumbufu wowote.

Mbali na hayo alisema kuwa Mfumo wa  (TIPS) unategemewa kuondoa changamoto mbalimbali za malipo jumuishi yanayofanywa na mitandao ya simu  na kuleta jukwa moja la mfumo utakaowezesha malipo ya haraka na yenye faida kwa watumiaji.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi