Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bodaboda, Machinga Wavikubali Vifurushi vya Bima ya Afya
Jan 11, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_50113" align="aligncenter" width="750"] Makamu Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoa wa Mwanza Bw. Gerald Nyerembe akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya bima ya afya Mkoani Mwanza, ambapo alisema wamelipokea vyema suala la vifurushi vya Bima ya Afya kwani ni muhimu kwa afya zao.[/caption] [caption id="attachment_50112" align="aligncenter" width="750"] Makamu Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Mwanza Bw. Joseph Samwel akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya bima ya afya Mkoani Mwanza, ambapo alisema suala la vifurushi limekuwa kuwa mkombozi kwa machinga.[/caption]

Na Mwandishi Wetu

Jumuiya za Wajasiriamali wadogowadogo na Waendesha Bodaboda nchini wamepongeza hatua ya kuanzishwa kwa vifurushi vya bima ya afya ambavyo vimewawezesha katika kupata matibabu ya uhakika pindi wanapoumwa.

Wakiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya Bima ya Afya viongozi wa jumuiya hizo wamesema ilikuwa ni hitaji lao la muda mrefu la kuhakikisha wanachama wao wanakuwa na uhakika wa matibabu kwa kuwa na bima za afya.

“Tunamshukuru sana Mhe. Rais Magufuli na serikali ya awamu ya tano kwa kuwa na maono ya kuhakikisha machinga nasisi tunakuwa na uhakika wa matibabu, awali ilikuwa ni ngumu sana unaenda hospitali ukiwa na hofu ya gharama lakini kwa sasa tunatembea kifua mbele, tunapata tiba popote nchini kwa vifurushi hivi”-Stephen Lusinde Mwenyekiti wa Machinga Taifa

[caption id="attachment_50108" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Mhe. Anne Makinda akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya bima ya afya Mkoani Mwanza, ambapo alisema mpango wa vifurushi umekuja kwa ajili ya kuwajumuisha watanzania wote.[/caption]

Naye Mwenyekiti wa Bodaboda Taifa Bw. Michael Haule amesema kuwa ujio wa mpango huu wa vifurushi ni uthibitisho kwamba serikali ya awamu ya tano kila mtu ni sawa na ndio maana wao kama bodaboda sasa wamewekewa utaratibu rahisi wa kujiunga na vifurushi vya bima ya afya kwa gharama nafuu kabisa.

“Zamani ilikuwa ni ngumu sana kumkuta bodaboda anamiliki kadi ya bima ya afya, bodaboda wengi wawepoteza maisha kutokana na kukosa huduma bora za matibabu kutoka na ajali, ila kwasasa suala hilo ni historia, bodaboda sasa ni kama wafalme tunajidai na kadi zetu”- Michael.

[caption id="attachment_50110" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Mhe. Anne Makinda akitoa kadi za bima za afya kwa wanachama waliojiunga kwa mpango wa vifurushi, leo Mkoani Mwanza.[/caption]

Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoa wa Mwanza Bw. Gerald Nyerembe alisema kuwa wamelipokea suala la vifurushi kwa kuwa ni muhimu kwa afya zao na wanafarijika sana kwa Serikali kuwatambua kwani bima imekuwa na faida kubwa kwao.

Aidha, Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Mwanza Bw. Joseph Samwel amesema suala la vifurushi limekuja kuwa mkombozi na kuokoa maisha ya wajasiriamali wadogo kwani bila afya hakuna maendeleo hivyo wajasiriamali hawana budi kuliona suala la vifurushi kama mkombozi.

[caption id="attachment_50111" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja wanachama waliojiunga kwa mpango wa vifurushi, leo Mkoani Mwanza.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi