Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bilioni 67.9 Zatumika Kujenga na Kuboresha Miundombinu ya Elimu TIA
Sep 07, 2026
Bilioni 67.9 Zatumika Kujenga  na Kuboresha Miundombinu ya Elimu TIA
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Amos Pallangyo, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, katika ukumbi wa Idara ya Habari - MAELEZO, kuhusu utekelezaji wa Taasisi hiyo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2025/26 na mwelekeo wa 2026/27.
Na Bupe Mwaiseje - MAELEZO

Serikali  kupitia Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) imewekeza kiasi cha shilingi bilioni 67.9 ili kuboresha na kujenga miundombinu ya taasisi hiyo kutoa elimu, kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi unaowawezesha kuajiriwa na kujiajiri.

Hayo yamesemwa Septemba 7, 2026 na Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Prof. William Amos Palangyo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari–MAELEZO, Mtumba jijini Dodoma,  kuelezea utekelezaji wa taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27 ambapo amesema uwekezaji huo umeelekezwa katika kuboresha miundombinu kwenye kampasi za Mtwara, Mbeya, Singida, Kigoma, Mwanza na Zanzibar.

Amesema uwekezaji huo umechangia ongezeko la kampasi kutoka sita mwaka 2021/22 hadi nane mwaka 2025/26, huku idadi ya wanafunzi ikiongezeka kutoka 24,494 hadi 37,397, sawa na ongezeko la asilimia 52.7.

Ameeleza kuwa katika kipindi hicho, wanafunzi 19,342 katika kampasi saba wamefaidika na mikopo ya elimu ya juu, huku jumla ya wahitimu 62,680 wakihitimu na kuingia katika soko la ajira na ujasiriamali.

Prof. Palangyo amebainisha kuwa kati ya fedha hizo, Sh bilioni 27.8 zimetolewa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), huku Sh bilioni 45.2 zikitolewa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha kwa ajili ya miradi katika kampasi za Mwanza, Kigoma, Zanzibar, Mbeya na Mtwara.

Ameongeza kuwa TIA imeongeza programu za masomo kutoka 49 hadi 54, huku Serikali ikiwezesha taasisi hiyo kupata maprofesa tisa na kugharamia watumishi 78 kusoma Shahada za Uzamivu (PhD), ambapo 48 tayari wamehitimu.

Aidha, katika kuunganisha elimu na ujasiriamali, Prof. Palangyo amesema zaidi ya wanafunzi 5,000 wamefikiwa kupitia mafunzo ya ujasiriamali, ubunifu, ajira na fursa za kimataifa, huku zaidi ya wanafunzi 500 wakipata mafunzo mahsusi ya ujasiriamali na takribani 100 wakisaidiwa kuanzisha biashara.

Prof. Palangyo amewataja baadhi ya wahitimu walionufaika kuwa ni Nicolaus Carol Mboya aliyeanzisha Kampuni ya STEAMORA , kampuni inayotoa mafunzo ya teknolojia ya elimu, mafunzo ya roboti, Kuandaa vijana wenye uwezo wa kupanga programu na kuandika maelekezo au maagizo maalum kwa lugha ambayo kompyuta au kifaa cha kielektroniki kinaweza kuelewa na kutekeleza wa kompyuta (coding), ubunifu wa miundo ya pande tatu (3D) na akili bandia kwa watoto na vijana.

Kampuni hiyo tayari imewafikia zaidi ya wanafunzi 600, ina watumishi wanane na imezalisha zaidi ya Sh milioni 15.
 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor