Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bilioni 175.6 Kuleta Neema ya Maji Mjini Morogoro
May 27, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_52808" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James akibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo wa masharti nafuu na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa hapa nchini, Bi. Stephanie Mouen ESSOMBE, mkopo huo utawezesha Manispaa ya Morogoro kunufaika na mradi wa maji wa Bilioni 175.6[/caption]

Na Mwandishi Wetu- Dodoma

Shilingi bilioni 175.6 kutatua changamoto ya maji  mjini Morogoro ikiwa ni moja ya hatua za Serikali ya Awamu ya Tano kuwapatia wananchi huduma bora za maji safi na salama katika maeneo yote.

Akizungumza leo June 27, 2020 jijini Dodoma wakati wa kutiliana saini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Doto James amesema kuwa utekelezaji wa mradi huu utawezesha wakazi wapatao 722,000 kupata maji safi na salama katika mji huo.

“ Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda kutoa shukrani

za dhati kwa Serikali ya Ufaransa  kupitia AFD kwa ushirikiano mzuri uliopo unaowezesha kutekelezwa kwa miradi mingi ya maendeleo kwa mikopo ya masharti nafuu”, alisisitiza Bw. James.

Akifafanua amesema kuwa upatikanaji wa maji utaongezeka katika mji wa Morogoro kutoka mita za ujazo 33,000 kwa siku hadi kufikia mita za ujazo 89, 000 kwa siku baada ya kukamilika kwa mradi.

[caption id="attachment_52809" align="aligncenter" width="750"] . Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Doto James akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kutiliana saini makubaliano ya mkopo wenye masharti nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa leo Mei 27, Jijini Dodoma.[/caption]

Kwa upande wake  Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo katika mji wa Morogoro utatatua changamoto ya maji kwa wakazi wake na kuchochea maendeleo.

“Miradi  ya maji  1423 inatekelezwa kote nchini huku 792 imekamika na inatoa huduma kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli ambapo mwaka 2015 aliahidi kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji vijijini na mijini”, alisisitiza Prof. Mkumbo.

Akifafanua amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo utoa fursa za ajira kwa watanzania na viwanda vya ndani vitaweza kunufaika kwa kuzalisha  mabomba na vifaa vingine vinavyohitajika katika mradi huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa hapa nchini, Bi. Stephanie Mouen ESSOMBE  amesema kuwa Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Akifafanua amesema kuwa mradi huo utawezesha wakazi wa Manispaa ya Morogoro kufikiwa na huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 90 ifikapo mwaka 2025.

AFD imeshatoa bilioni 655 katika kipindi cha miaka 10 katika sekta ya maji hapa nchini na hivyo kuchochea maendeleo.

  [caption id="attachment_52810" align="aligncenter" width="750"] . Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James (kushoto) akitiliana saini na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa hapa nchini, Bi. Stephanie Mouen ESSOMBE mkopo wa masharti nafuu utakowezesha Manispaa ya Morogoro kunufaika na mradi wa maji wa Bilioni 175.6[/caption] [caption id="attachment_52811" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kutiliana saini makubaliano ya mkopo wenye masharti nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa leo Mei 27, Jijini Dodoma, makubaliano ya mkopo huo yametiwa saini Jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Doto James na Shirika la Maendeleo la Ufaransa.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi