[caption id="attachment_38720" align="aligncenter" width="937"] Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akifafanua jambo kwa Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen wakati Balozi huyo alipomtembelea mapema leo, Desemba 10, 2018 ofisini kwake Dodoma, kujadili fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati.[/caption]
Na Veronica Simba - Dodoma
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen leo Desemba 10, amemtembelea Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma na kufanya mazungumzo kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya nishati nchini.
Balozi Jacobsen amemweleza Naibu Waziri kuwa kampuni mbalimbali nchini mwake zina nia ya kuwekeza katika sekta ya nishati nchini na baadhi yake ziko katika hatua nzuri kwani tayari zimewasilisha serikalini mchanganuo wake unaoainisha sifa walizonazo wakisubiri zoezi la kushindanishwa na kampuni nyingine ili kupata zabuni husika za uwekezaji.
[caption id="attachment_38721" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen baada ya mazungumzo yao kujadili fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati mapema leo, Desemba 10, 2018 Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma.[/caption]“Mojawapo ya kampuni hizo ina nia ya kuwekeza katika uzalishaji wa umeme wa upepo eneo la Makambako, ambapo ni ubia baina yake (52%) na wazawa (48%),” amesema Balozi.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Mgalu amemshukuru Balozi Jacobsen ambaye ni mwakilishi wa Serikali ya Norway kutokana na ushirikiano ambao nchi hiyo imekuwa ikiuonesha kwa Tanzania ikiwemo uwekezaji nchini na pia kufadhili wanafunzi katika masomo ya fani za gesi na mafuta.
Aidha, amemweleza Balozi huyo kuwa bado zipo fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya nishati nchini na hivyo ametumia fursa hiyo kuendelea kukaribisha kampuni mbalimbali za Norway kuja kuwekeza.
[caption id="attachment_38722" align="aligncenter" width="677"] Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) akiagana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen, baada ya mazungumzo yao kujadili fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati mapema leo, Desemba 10, 2018 Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma.[/caption]