Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Atakayefanya Udanganyifu Mitihani Darasa la Saba Kufukuzwa
Sep 05, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na Tiganya Vincent - Sikonge

WATUMISHI na Askari watakaosimamia mtihani wa kumaliza Darasa la Saba unaonza kesho(leo) wameagizwa kuhakikisha wanazingatia taratibu na sheria zinazoongoza usimamizi mitihani hiyo hapa nchini ili kuepuka vitendo vya udaganyifu wakati wa ufanyaji wa mitihani na ambavyo vinavyoweza kutia doa zoezi hilo.

Kauli hiyo imetolewa jana wilayani hiyo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akiongeza na askari walipangwa kulinda vituo mbalimbali vya kufanyia mitihani.

Alisema kuwa  mtu yoyote atakayebainika kuhusika katika vitendo vitakavyosababisha udanganyifu na kupelekea mitihani kuvuja atafukuzwa kazi na kufikisha Mahakamani.

Mwanri aliwataka kujiepusha katika kujiingiza katika vitendo vyovyote vitakavyoashiri kuvunjwa kwa taratibu na sheria za usimamizi wa mitihani ya taifa.

Alisema kuwa lengo la Mkoa wa Tabora ni kupata matokeo mazuri ya watoto wanaomaliza darasa la saba ambayo yatakuwa ya kweli na juhudi binafsi za mwanafunzi kupitia mafundisho aliyopata na sio kutumia udanganyifu.

Mkuu huyo Mkoa wa Tabora aliwatakia kila la kheri watoto wote wanaoanza mtihani wao wa kumaliza darasa la saba kufanya mitihani yao kwa weledi na uaminifu ili wapate matokeo wanayostahili.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi