Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Anga la Tanzania kuwa Salama kwa Asilimia 100
Apr 02, 2018
Na Msemaji Mkuu

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa usimikaji wa mfumo wa rada nne za kuongezea ndege katika viwanja vya ndege vya Kilimanjaro, Mwanza, Julius Nyerere na Songwe. Hafala hiyo ilifanyika leo Jumatatu April 2, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu-MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa kukamilika kwa mradi wa usimikaji wa mfumo wa Rada mpya katika viwanja vinne vya ndege nchini, kutalifanya anga la Tanzania kuwa salama kwa asilimia mia moja.

Rais Magufuli amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa usimikaji wa mifumomya rada nnez itakazosimikwa katika kiwanja Kimataifa cha cha Julius Nyerere cha Jijini Dar es Salaam, Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA), Kiwanja cha ndege cha Mwanza na kiwanja cha ndege cha Songwe.

“Rada ni chombo muhimu sana kwa usalama wa nchi hivyo ningependa kuona mradi huu unasimamiwa vizuri na kukamilika kwa wakati”, alieleza Rais Magufuli.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari akitoa maelezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ujenzi wa mfumo wa wa rada nne za kuongezea ndege wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa mfumo huo leo Jumatatu April 2, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Ili kuhakikisha rada hizo zinafungwa kwa kwa wakati, Rais Magufuli ameitaka kampuni ya Thales Las France SAS ya Ufaransa kuhakikisha inakamilisha mradi huo kwa wakati. Sambamba agizo hilo, Rais pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kumsimamia mkandarasi wa jengo katika uwanja wa ndege wa Mwanza kukamilisha kazi ya ujenzi wa jengo hilo haraka ili asicheleweshe mradi wa usimikaji wa mfumo wa rada.

Ameeleza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa rada hizo kutalifanya anga la Tanzania kuwa salama kwa asilimia moja tofauti na sasa ambapo rada pekee iliyopo katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, ina uwezo wa kuona asilimia 25 tu ya anga la Tanzania.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu , Mhe. Selemani Kakoso katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa usimikaji wa mfumo wa rada nne za kuongezea ndege katika viwanja vya ndege vya Kilimanjaro, Mwanza, Julius Nyerere na Songwe. Hafala hiyo ilifanyika leo Jumatatu April 2, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Kutokana na kuwa na rada moja tu yenye uwezo mdogo, Tanzania imekuwa ikipoteza takribani bilioni 1.2 ya tozo kwa mwaka na kwamba kutokana na uwezo huo mdogo, Shirika linalosimamia Usalama wa Anga Duniani (ICAO) lilikasimu sehemu ya anga la Tanzania kwa Kenya.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ameeleza kuwa mradi huo unagharamiwa na Serikali kwa asilimia 100 ambapo kati ya hizo, Serikali kuu inatoa milioni 55 wakati asilimia 45 zilizobaki zinatolewa na Mamlaka ya Usalama wa Anga Tanzania (TCAA).

Ameeleza kuwa sekta ya usalama wa anga nchini imeendelea baada ya TCAA kufaulu vizuri katika usalama wa anga duniani ambapo imepanda kutoka asilimia 37.8 mwaka 2003 hadi kufikia asilimia 68.35 mwaka 2017 ikiwa ni asilimia nane zaidi juu ya kiwango kinachokubalika kimataifa ambacho ni asilimia 60.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa usimikaji wa mfumo wa rada nne za kuongezea ndege katika viwanja vya ndege vya Kilimanjaro, Mwanza, Julius Nyerere na Songwe. Hafala hiyo ilifanyika leo Jumatatu April 2, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Akiongea mapema, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema kuwa mradi huo ambao utakamilika mwezi Mei 2019, unagharimu shilingi bilioni 67.3 ambapo asilimia 20 ya gharama hizo imeishalipwa kutokana na fedha za ndani za mamlaka hiyo.

“Mradi huu pia utasaidia kurahisisha huduma za utafutaji na uokoaji kunapotokea ajali za ndege, utaiwezesha nchi kukidhi viwango na miongozo ya shirika la Kimataifa la Isafiri wa Anga na kujenga Imani ya watumiaji wa anga letu na kuendana na ushindani katika ukanda wa Afrika na dunia kwa ujumla,” ameeleza Johari.

Mradi wa ujenzi wa rada nne za kisasa unatarajia kukamilika mwezi Mei mwaka 2019 na utaifanya Tanzania kuwa na uwezo wa kusimamia usalama wa anga lake yenyewe na hivyo kuondoa uwezekano wa sehemu ya anga kukasimiwa kwa nchi zingine.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi