Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wamiliki wa Viwanda Watakiwa Kutoa Kushirikiano NBS
Jan 24, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_50339" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akihutubia Wafanyakazi wa Ofisi wa Taifa ya Takwimu alipokuwa akifungua Mkutano wa Tatu wa Baraza la Tano la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo uliofanyika kwenye leo tarehe 23 Januari, 2020 Jijini Dodoma.[/caption]

Na: Mwandishi Wetu

Wamiliki wa Viwanda nchini wametakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ili kukuza sekta hiyo ambayo imekuwa ni chachu ya maendeleo kwa Taifa.

Maagizo hayo yametolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipokuwa akifungua Mkutano wa Tatu wa wa Baraza la Tano la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu ambapo alipokea taarifa ya changamoto ambazo Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imekuwa ikikabiliana nazo ikwemo suala la wenye viwanda kutokutoa ushirikiano wakati ofisi hiyo inapokusanya takwimu viwandani.

Waziri Mhagama alieleza kuwa Serikali imejiwekea mikakati maalumu katika kukuza sekta ya viwanda, ili kufikia maendeleo ya sekta hiyo taarifa sahihi zenye takwimu zilizochakatwa ni muhimu zikawepo katika kufanya maamuzi stahiki na kupanga mikakati ya maendeleo.

“Ili kufikia lengo la kuinua uchumi wa nchi, ni muhimu wenye viwanda wakatambua umuhimu wa uwepo wa takwimu sahihi ambazo zitaleta tija na ustawi wa sekta hiyo na hayo yamejidhihirisha hasa kupitia dhamira ya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika kukuza uchumi wa nchi kupitia viwanda,” alieleza Mhagama

Aliongeza kuwa uwepo wa ushirikiano huo utaleta tija na ustawi wa sekta hiyo kutokana na upatikanaji wa taarifa za takwimu mbalimbali kuhusina na viwanda vilivyopo nchini ikiwemo tafiti za uzalishaji wa viwanda, kujua masula ya ajira, ujuzi ambao haupo nchini na umekuwa ukitoa ajira kwa wageni wa nje na pia kujua mahusiano ya ukuaji wa uchumi na sheria za kazi zinavyoshahabiana.

Sambamba hayo Waziri Mhagama ametoa maagizo kwa Kamishana wa Kazi kuhakikisha anashirikiana na kuwahusisha wataalamu wa takwimu wanapokuwa wanafanya kaguzi kwenye viwanda mbalimbali hapa nchi ili takwimu zitakazokuwa zinahitajika ziweze kupatina.

 “Jukumu kubwa mlilonalo wakati huu ni kuwapatia elimu ili watambue umuhimu wa kuwepo kwa takwimu za sekta hiyo na baada yah apo watakuwa na uelewa kuwa ni wajibu wao kutekeleza suala hilo kisheria,” alisema Mhagama

Naye Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa alieleza kuwa ushirikiano utakao kuwepo baina ya wataalamu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Idara ya Kazi na Wizara ya Viwanda na Biashara utasaidia kuimarisha njia bora ya ukusanyaji wa takwimu za sekta hiyo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi