[caption id="attachment_48754" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza kwa hotuba nzuri Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Mhe. Mkapa huku akishuhudiwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Marais wastaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Balozi wa Finland nchini Mhe. Antila Sinikka katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumanne Novemba 12, 2019[/caption]
Na Judith Mhina- MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amezindua kitabu cha maisha ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Willium Mkapa ambaye ametimiza miaka 81 ya kuzaliwa tangu tarehe 12 Novemba 1938 katika kijiji cha Lupaso Ndanda Masasi.
Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar-es-salaam, ambapo marais watatu wastaafu wa Jamhuri y a Muungano wa Tanzania Rais, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Jakaya Mrisho Kikwete, na mhusika Rais Benjamin Mkapa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein wamehudhuria hafla hiyo.
Akieleza jinsi Rais wa Awamu ya tatu kama shujaa na mwalimu wake katika maisha yake ya kisiasa Rais Magufuli amesema kuwa Mzee Mkapa ni Shujaa wangu safari iliyoanza wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, alipokuja katika jimbo langu lililokuwa linaitwa Biharamuro Mashariki na sasa Chato nikigombea ubunge.
Rais Magufuli aliongeza na amesema [ “Rais Mkapa aliwaambia wananchi wa Chato “Nileteeni kijana huyu” maneno haya yalitosha kuchaguliwa kuwa mbunge].
Akielezea safari yake ya siasa Rais Magufuli amesema kuwa mara baada ya uchaguzi nikachaguliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, chini ya Mama Anna Abdallah. Ambapo, Rais Mkapa alinifundisha kuwa jasiri, kujiamini pamoja na hata pale nilipokuwa nakutana na vikwazo katika kazi alinitia moyo, kwake hakuna mkubwa wala mdogo cha msingi na kufanya kazi.
Pia katika uongozi wa Mzee Mkapa nilijifunza akielezwa jambo hulisikiliza hulikubali, hulisimamia na kuhakikisha linatekelezwa. Na pale linapoharibika husimama na wewe hakuachi peke yako Mfano ni ubomoaji wa nyumba za Kimara-Ubungo na serikali kupelekwa kwenye vyombo vya sheria.
Mzee Mkapa ni mwaminifu na hageuzi maamuzi yake nakumbuka nilipeleka Waraka na ushauri katika Baraza la Mawaziri mapendekezo ya kuomba serikali kutenga fedha za Tanzania shilingi Bilioni 1.85. Japo Mawaziri wengi walipinga jambo hili waraka ulipita na wakati huo Waziri wa fedha alikuwa Mhe. Basil Mramba aliaanza mara moja kutenga kila mwezi fedha hizo na huo ukawa mwanzo wa kujenga barabara na madaraja kwa kutumia fedha za ndani
Katika kitabu chake cha maisha binafsi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu – My Life My Purpose A Tanzanian President Remembers ukurasa wa 115, Mzee Mkapa ameonyesha furaha yake kwa kazi nzuri niliyofanya huwa hana kificho na kusema mimi ni askari wake wa mwamvuli namba moja, jambo hili liliniletea shidaa na kudhuru afya yangu.
Baada ya tukio hilo la kunusurika nilikwenda kwake kwa lengo la kutaka kujiuzulu lakini aliniangalia kwa jicho la Baba na Mwana na kunipa ujasiri kukaa kimya kwa muda na kuniambia “John nenda kufanye kazi kamtangulize Mungu” alinipa matumaini na kujifunza kutowasifia wateule wangu maana ina waletea madhara baadaye.
Jambo lingine ambalo siwezi kumsahau Mzee Mkapa ni wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais wa mwaka 2015 nilikwenda kwa Mzee Mwinyi, Kikwete na Mkapa. Kwa kuwa leo ni siku ya Mzee Mkapa nipeni ruhusa nielezee ya Mzee Mkapa.
Kwanza kabisa niipokwenda kwa Mzee Mkapa nikagundua wagombea wenzangu wa Chama Cha Mapinduzi- CCM, karibu wote walishakwenda huko kueleza nia yao ya kugombea urais. Mimi nilikwenda kwa Mzee Mkapa kumueleza dhamira yangu ya kutaka kugombea urais
Nakumbuka maneno yake nanukuu “John kamtangulize Mungu, kama dhamira yako itakubalika na Mwenyezi Mungu itawezekana kinyume chake hutafanikiwa, haitawezekana” mwisho wa kunukuu.
Kusema kweli nilichanganyikiwa kidogo nisimuelewe amemaanisha nini kwa sababu binafsi nilitarajia ataniunga mkono au la. Hata hivyo nilichukua uamuzi wake wa kumtanguliza Mungu na hatimaye nikachaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya nchi yetu ya Tanzania asante sana Mzee Mkapa . Alisema Rais Magufuli.
Akirejelea sifa za Mzee Mkapa Rais Magufuli amesema “Nilipomfahamu nimegundua ni mcha Mungu ni mtu mwenye kumtanguliza mungu, mtu mwenye msimamo, kujiamini na anajua muelekeo anaoutaka ana upendo wa kweli na sio mnafiki, mtulivu kwa mambo ya kitaifa, mzalendo, mwanafunzi mwadilifu wa sera na falsafa za Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na pia ni mwana diplomasia”
Wakati wa uongozi wake nchi yetu ilipata mafanikio mengi makubwa ikiwemo kusamehewa deni la Dola za marekani bilioni tatu, kati ya fedha tulizodaiwa bilioni saba na Benki ya Dunia – IMF. Pia, serikali iliweza kuongeza mapato kutoka Dola za Marekani 912, 587 mwezi Desemba mwaka 1995 hadi Dola 1,769,862 kufikia Desema 2005.
Wakati Mzee Mkapa anaingia madarakani akiba ya fedha wakati 1995 ilitosha kwa mwezi mmoja mpaka akiondoka ameacha fedha zinazotosha kuendesha serikali kwa miaezi mitano (5)
Mzee Mkapa ameanzisha Mpango wa Kukuza na Kurekebisha Uchumi Tanzania – MKUKUTA. Mpango wa Kurasimisha Raislimali na Biashara za Wanyonge Tanzania – MRABITA. Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania –TASAFambao ulisaidia kupunguza umasikini.
Pia, uanzishwaji wa Taasisi za kutoa huduma kama vike Bima ya Afya Tanzania- NHIF, Wakala wa Barabara Tanzania -TANROADS iliyoimarisaha miundombinu, ambazo zimeboresha maisha ya watanzania kwa kasi kikubwa kuanzisha programu ya maendeleo ya elimu ya Msingi na Sekondari. Ambapo ilisaidia kuongeza idadi ya wanafnzi shuleni kutoka milioni 4.8 mwaka 1995 mpaka milioni 7.5 mwaka 2005.
Aidha aliendelea kutunza amani na umoja wa watanzania tunakushukuru sana Mzee Mkapa Binafsi nimefarijika sana kwa kuweza kuandika hiki kitabu. Ni matumaini yangu mWito kwa Watanzania
Katika sura ya kwanza na ya pili Mzee mkapa amegusia masuala ya Imani na kufanya kazi hii inadhihirisha ni mcha Mungu na amelelewa katika misingi ya Mungu. Sura zinazofatoa ameeleza safari yake ya maisha na katika kupata nafasi mbalimbali za uongozi.
Binafsi mimi nimevutiwa na Sura ya 11 Mageuzi endelevu yasiyo na ukomo na Sura ya Jitihada za kuondokana na utegemezi, ambapo kwa sasa serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza kwa ufanisi na bidii kubwa kwa kutumia fedha zetu za ndani katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akiongea na hadhira hiyo Rais Msataafu wa Awamu ya Tano Mhe. Benjamin Willlium Mkapa amesema alianza kwa kutoa shukurani kwa watanzania kwa kupewa heshima kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Tatu.
Aidha, amesema kuwa uwepo wa marais watatu wastaafu nchini Tanzania ni tunu ya pekee tuliyojaliwa watanzania, pia kwa nchi ya Tanzania nafasi ya rais inaweza kushikwa na mtu yeyote anayejaliwa na Mwenyezi Mungu.
Tatu, mimi nimejaliwa kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa muda mrefu ambapo amenipa mimi nafasi mbalimbali za uongozi na kunisaidia katika kazi yangu ya urais. Nimeshiriki kikamilifu katika kazi ya ukombozi wa Afrika na naamini A future leader will be born with natural” nimenufaika sana na Mwalimu kama mentor wangu” Amesema Rais Mstaafu Mkapa.
Akiongelea sula la kujitegemea Rais Mstaafu Mkapa amesema Kujitegemea ni jambo la muhimu sana nampongeza sana Rais wetu Magufuli kwa hatua ya kuhakikisha miradi mingi ya maendeleo inatekelezwa kwa fedha zetu.
Nne ni jmbo zuri kuwa na utamaduni wa kukusanya kodi “Time Development is Self Development “ Hii imetujengea heshima katika taifa letu
Mwisho alimalizia kwa kueleza changamotokadhaa alizokumbana nazo katika uongozi akisema kuwa kuma matokeo chanya na hasi ambapo wtanzania wanaweza kusoma kitabu chake na kuepuka changamoto hizo kwa kuwa watakuwa tayari wamejifunza kutokana na kile kilichotokea wakati wa uongozi wake.
Naye Profesa Joseph Semboja wa Taasisi ya Chuo cha Uongozi au Uongozi Istitute akielezea jinsi Taasisi yake ilivyoshiriki katika kuhakikisha kitabu hicho kinaandikwa amesema kuwa Rais Msataafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Willium Mkapa ameandika kitabu ambacho kihalisia sio cha familia ya Rais Mkapa bali ni historia ya nchi.
Akichambua kitabu hicho Prof. Rwaikaza Mukandara wa Taasisi ya Kigoda cha Mwalimu Nyerere amesema kuwa kitabu cha Mzee Mkapa kimeeleza maisha yake binafsi, tangu akiwa kijana mdogo hadi sasa.
Kitabu hiki kimegharimu Dola za Marekani laki moja sawa na fedha za Tanzania milioni 200. Pia, kitabu kina jumla ya kurasa 319 na kinauzwa kwa bei nafauu na kinapatikana katika baadhi ya mikoa mingi ya Tanzania.
Mwisho kabisa amewashauri Watanzania kuwa na Tabia ya kujisomea vitabu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuandika ili kuiweka historia iendelee kuishi kutoka kizazi kimoja hadi kingine na kuwafanya vijana wetu kujua wapi tulipotoka tulipo na tunapokwenda.