Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mkakati wa Serikali ni Kuhakikisha TBC Inasikika Nchi Nzima: Mhe.Shonza
Sep 09, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_46620" align="aligncenter" width="803"] Naibu Waziri wa Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akijibu maswali leo Bungeni Jijini Dodoma.[/caption]

Shamimu Nyaki – WHUSM

Naibu Waziri wa Habari, utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amesema kuwa mkakati wa Serikali ni kuhakikisha kuwa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) linafikia usikivu katika maeneo yote ya nchi.

Mhe.Shonza ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la  Mbunge wa Sikonge Mhe.Joseph Kakunda  aliyeuliza Je. Kuna sababu zipi zinazosababisha matangazo ya TBC hasa upande wa redio yasisikike kwenye tarafa ya kitunda na maeneo mengi ndani ya Jimbo la Sikonge. Na Je ni lini Serikali itarekebisha tatizo hilo.

Akijibu swali hilo Mhe.Juliana Shonza amesema kuwa TBC inaendelea na mpango wa kupanua usikivu nchi nzima kutegemeana na Bajeti ili kukamilisha Wilaya zote  59 ikiwemo Sikonge, Aidha TBC ina mpango wa kufanya maboresho katika mitambo yake iliyopo Tabora (Kaze Hill) kisha kufanya tathmini ya usikivu na kubainisha maeneo yanayopaswa kufungwa mitambo mingine ili kuleta usikivu mkoa wote.

“Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2019/20 TBC inaendelea kutekeleza Mradi wa upanuzi wa usikivu katika maeneo ya Mikoa ya Unguja, Pemba, Simiyu,Njombe, Songwe na Lindi”alisema Mhe.Shonza

Mhe.Naibu Waziri ameongeza kuwa katika bajeti ya mwaka 2016/17 ilitekeleza Mradi wa upanuzi wa usikivu katika wilaya tano zilizopo mpakani mwa nchi ambazo ni pamoja na Wilaya ya Longido,Rombo,Tarime,Nyasa Kibondo.

Aidha bajeti ya mwaka 2017/2018 TBC ilitekeleza Mradi wa upanuzi wa usikivu katika mkoa wa Mtwara na Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga ambapo hadi kufikia tarehe 04/05/2018 Shirika lilikua na vituo vya kurushia matangazo katika masafa ya FM kwenye Wilaya 102.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi